• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MKOA UTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA WADAU MBALIMBALI KATIKA UTEKELEZAJI WA MASUALA YA KINGA NA UDHIBITI WA MAJANGA YA MOTO

Imetumwa : October 27th, 2025

Na:Sofia Remmi.

Habari:Dodoma RS.

''Nitoe rai kwenu kuhakikisha kila mmoja anachukua hatua za kukinga na kudhibiti majanga ya moto''.

Ni kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mhe. Rosemary Senyamule Leo tarehe 27 Oktoba 2025 wakati wa Uzinduzi wa Mitambo ya  Zimamoto na Uokoaji.

Amesema  Mitambo hiyo itasaidia kutoa huduma kwa haraka na ufanisi kwani kwa kipindi cha mwaka 2025 kuanzia Januari hadi leo kumekuwa na matukio 252, matukio ya moto 176 na maokozi 76 sawa na wastani wa asilimia 68, hivyo mapokezi ya mitambo  hiyo yatasaidia kuongeza ufanisi na kukabiliana na matukio hayo bila kuleta madhara kwa binadamu pia  yatasaidia kufika katika uwanda mpana.

“Mitambo na magari yatatuwezesha kukabiliana na dharura kwa haraka na ufanisi zaidi, hivyo kuokoa maisha na mali. Kuimarisha Usalama: Kwa vifaa vya kisasa, tutaweza kudhibiti na kuzuia majanga kwa ufanisi zaidi, hivyo kuimarisha usalama wa jamii yetu.

Mitambo hii itaweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kwa kasi zaidi, hivyo kupunguza madhara yanayoweza kutokea,wakati mwingine kumekuwa kukitokea matukio ya moto, zaidi ya moja kwa wakati mmoja, hali inayopelekea changamoto katika utendaji na Utekelezaji wa majukumu haya kwa ufanisi. Upatikanaji wa mitambo hii utapanua wigo wa utoaji huduma kwa wananchi ukilinganisha na hali ya kipindi cha nyuma”Amesema Mhe. Senyamule.

Hata hivyo,Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe.Alhaji Jabil Shekimweli amesema "Tuna kila sababu za kumshukuru Mhe.Rais kwa kuleta miradi hii mikubwa ambayo kwa sasa kutokea ni jambo ambalo la kushangaza sana Kwani imewezesha mitambo ya kisasa,Vituo vya polisi,Vifaa na nyumba za askari. Hata hivyo vifaa hivyo tuvitunze kwa bidii ili kuendelea kudumu zaidi na zaidi".

Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto  Mkoa wa Dodoma Rehema Mende amesema Serikali imetoa Mitambo 08 ambayo itawezesha kufanya kazi kwa weledi mkubwa hata kama majanga yatatokea  katika maeneo 02 kwa wakati mmoja, vifaa vya Zimamoto na uokoaji vipo vya kutosha.


#DodomaFahariya Watanzania

#KeroyakoWajibuWangu

#Nimejiandikisha,NitapigaKura

#UmejiandikishaKapigeKura

#KuraYakoHakiYako,JitokezeKupigaKura

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MKOA UTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA WADAU MBALIMBALI KATIKA UTEKELEZAJI WA MASUALA YA KINGA NA UDHIBITI WA MAJANGA YA MOTO

    October 27, 2025
  • STAKABADHI GHALANI KURAHISISHA BIASHARA KWA MFUMO WA HAKI NA UWAZI

    October 25, 2025
  • SUALA LA AMANI SI LA KISERIKALI TU BALI NI LA KIIMANI KUPITIA VITABU VITUKUFU

    October 26, 2025
  • WAHITIMU WA ELIMU YA JUU WAASWA KUCHANGAMKIA FURSA ZILIZOPO DODOMA

    October 23, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.