• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

BAHI WAJIVUNIA BILIONI 52, MIAKA 4 YA RAIS SAMIA

Imetumwa : June 3rd, 2025

Na. Sizah Kangalawe

Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Bw. Kaspar Mmuya  ameeleza mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Wilaya ya Bahi, akibainisha kuwa zaidi ya Bilioni 52 zimetolewa katika Halmashauri hiyo  kwa  kipindi cha miaka minne ya uongozi wake  Mhe. Dkt.  Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza katika maadhimisho ya “Samia Day” katika kata ya Zanka, wilaya ya Bahi ,mkoani Dodoma, Mmuya amesema kuwa fedha hizo zimetolewa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo inayolenga kuboresha maisha ya wananchi katika sekta  mbalimbali,zikiwemo za elimu, afya, maji, na kilimo.

"Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia, Wilaya ya Bahi imenufaika na zaidi ya shilingi bilioni 52 ambazo zimeelekezwa katika miradi ya maendeleo inayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja.

Aliongeza kuwa fedha hizo zimewezesha ujenzi wa miradi ya maendeleo ikiwemo, shule, vituo vya afya, visima vya maji safi na salama, pamoja na kuwapatia wakulima pembejeo kwa lengo la kuwawezesha kufanya kilimo chenye tija.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Joachim Nyingo amesema wamekusanyika kuelezea mazuri yanayofanywa na Rais na kutoa rai kwa wananchi wa Wilaya hiyo kutumia vizuri fursa zinazotokana na Miradi mbalimbali inayotekezwa.

‘’Zaidi ya Bilioni 7 zimetolewa katika kata ya Babayu iliyopelekwa kwenye miradi ya kata hii, ni matumaini yangu Wananchi  wa Wilaya ya Bahi wameona juhudi za Mhe. Rais, nitoe rai kwa wananchi kutumia vizuri fursa zinazotolewa na Kiongozi wetu pamoja na kulinda amani bila kusahau kushiriki kikamilifu katika uchaguzi Mkuu" Alisema Mhe. Nyingo

Nao wananchi wa Wilaya ya Bahi wameeleza kufurahishwa na juhudi hizo za serikali, wakisema kuwa zimeleta mabadiliko chanya katika mzunguko wa maisha yao  ya kila siku.

"Tunaishukuru Serikali kwa kutuletea maendeleo haya ikiwemo umeme ambao ulikuwa ni changamoto kubwa katika  eneo letu kwa siku za nyuma na kupelekea matatizo mbalimbali ikiwemo changamoto ya uhalifu ambayo kwa sasa imepungua kwasababu ya uwepo wa umeme katika maeneo haya’’ .Alisema John Yohana mkazi wa Kata ya Zanka.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa wazee wa chama cha mapinduzi CCM wilayani hapo Gilbeart Kizenga alisema Serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imefanikiwa kuimarisha ulinzi na usalama nchini, hali inayowezesha wananchi kutekeleza shughuli zao za kila siku kwa uhuru na amani, kwa kuzingatia sheria za nchi.

Amesema kwa kupitia maboresho yaliofanywa na Serikali katika sekta ya ulinzi yamepelekea  Wananchi kuweza  kufanya shughuli zao bila hofu, mradi tu wanafuata sheria na taratibu zilizowekwa.

'Samia day’ 2025 imefanyika kwa mara ya kwanza kwenye kata zote za Mkoa wa huu,ambapo wananchi wa Kata hizo kwa kushirikiana na viongozi wao,wamefanya shughuli mbalimbali ili kuipamba  siku hii muhimu iliyoandaliwa kwa lengo la kumshukuru na Kumpongeza Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • ‘iMES’ KUTATUA CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI WA TAARIFA ZA KADA YA MAENDELEO YA JAMII MKOA WA DODOMA

    June 06, 2025
  • BAHI WAJIVUNIA BILIONI 52, MIAKA 4 YA RAIS SAMIA

    June 03, 2025
  • WATAALAMU WA ELIMU NGAZI YA HALMASHAURI WANADHAMANA YA KULETA TIJA KWA TAIFA

    June 04, 2025
  • MRADI WA ‘YEFFA’ MKOA WA DODOMA WAIBUA VIJANA WANUFAIKA 84,590 MKOA WA DODOMA

    June 04, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.