• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DARAJA LA BILLIONI 1.5 KUONDOA DARAJA LA KAMBA KONDOA

Imetumwa : November 23rd, 2023

Wananchi wa kijiji cha Hurui kata ya Kikore Wilayani Kondoa  Mkoani Dodoma wamesema ujenzi wa daraja la kisasa lenye thamani ya shilingi bilioni 1.5 linalotarajiwa kukamilika mwisho mwa mwezi Disemba 2023 litatatua  kero ya muda  ya mrefu ya kutumia daraja la kamba kuvuka mto na  kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii  hali ambayo imekuwa ikisababisha baadhi ya watoto kutofika shule Pia   wakazi wa Kijiji hicho kushindwa kuuza mazao yao kutokana na kukosekana kwa miundombinu hiyo.

Hayo yamebainishwa Novemba 22,2023 baada ya Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) katika Timu iloyoongozwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ndg. Joketi Mwegelo na Wataalamu wengine wa Mkoa na Wilaya hiyo kufika katika daraja hilo  kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo.

Aidha Ndg. Mwegelo wakati akitembelea mradi wa Maji katika Kata ya Kisese amemtaka mkandarasi anaye tekeleza mradi huo kuanza ujenzi wa tanki ndani ya  siku saba awe ameshaanza utekelezaji wa mradi huo ili kutatua changamoto ya maji ambayo imekuwa mwiba mchungu kwa wananchi wa Kisese.Wito huo umetolewa baada ya kupita siku ishirini na moja ambazo mkandarasi alitakiwa awe eneo la mradi akiendelea na Ujenzi wa Mradi.

Hata hivyo Ndg. Mwegelo amesema licha ya Viongozi mbalimbali kuwachukulia hatua baadhi ya Viongozi ambao walikuwa wakitekeleza mradi huo lakini bado inaonekana kuendelea kusuasua jambo linalopelekea kucheleweshwa kwa ukamilishaji wa Mradi huo.

Pia, Katibu Mkuu huyo ametoa wito kwa wananchi wa kata ya Kikore na Kisese kupeleka watoto shule na kuachana na tabia ya kugeuza watoto kufanya kazi za ndani .

Mkoa wa Dodoma umekuwa wa 17 kufikiwa na  ziara ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT ) wakiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe.Mary Chatanda na Viongozi wengine ambapo wanatarajia kupita katika Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma ikiwa tayari wamesha kamilisha ziara yao Wilaya ya Kondoa kwa  kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM ) na maendeleo ya miundombinu mbalimbali pamoja na kusikiliza kero za wananchi wa Mkoa huo.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.