• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

ELIMU NI SILAHA MUHIMU KATIKA VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA NCHINI

Imetumwa : June 24th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Imeelezwa kuwa Elimu ni silaha muhimu katika vita dhidi ya dawa za kulevya, kwani uelewa unahitajika kuhusu madhara ya matumizi na biashara ya dawa hizo, njia za kukabiliana na uraibu na jinsi ya kupata msaada.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule Juni 24, 2025 alipokua akifungua rasmi maonesho kuelekea kilele cha maadhimisho ya   Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani, ambapo alifanya Mkutano na Waandishi wa Habari kuutangazia Umma juu ya maadhimisho hayo yanayofanyika kwenye  viwanja vya Jakaya Kikwete Jijini humu.

“Elimu ni silaha kubwa katika vita dhidi ya dawa za kulevya. Kupitia maonesho haya, wananchi watapata uelewa bora kuhusu madhara ya matumizi ya dawa za kulevya, njia za kukabiliana na uraibu na jinsi ya kupata msaada”.

Kadhalika, Mhe. Senyamule amesema kuwa maadhimisho hayo yanalenga kupaza sauti kwa Umma juu ya madhara ya dawa za kulevya, hatua zilizofikiwa na mipango endelevu ya Serikali katika kudhibiti na kupambana na tatizo hilo huku yakiambatana na shughuli mbalimbali za udhibiti kutoka kwa Wadau wanaoshiriki katika mapambano hayo.

Aidha, ameongeza kuwa, Dawa za Kulevya ni janga linaloathiri familia nyingi Nchini hivyo, ni muhimu kwa Wananchi kushiriki katika maonesho hayo ili kupata elimu kufahamu njia za kukabiliana na tatizo hilo sambamba na kuwasaidia waliothiriwa na dawa hizo.

Mwezi Juni kila mwaka, Dunia huadhimisha siku ya Kupiga vita dawa za kulevya, Maadhimisho ambayo hufanyika kwa siku tatu mfululizo (24, 25 na 26) na mwaka huu yanafanyika Mkoani hapa katika kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.


#drugday

#wekezakwenyekinganatibadhidiyadawazakulevya

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RAIS DKT. SAMIA ASISITIZA KUIMARISHWA KWA KILIMO ILI KUJIHAKIKISHIA USALAMA WA CHAKULA

    June 28, 2025
  • SERIKALI IMEJIZATITI KULETA MAENDELEO KWA KUIMARISHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA BIASHARA

    June 25, 2025
  • TANZANIA SIYO SALAMA KWA WAUZAJI , WASAFIRISHA, WALIMAJI NA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA” - MHE. MAJALIWA

    June 26, 2025
  • SHUGHULI ZA KIBINADAMU ZATAJWA KUWA TISHIO KWA CHANZO CHA MAJI BONDE LA MAKUTUPORA JIJINI DODOMA

    June 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.