• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

ELIMU YATOLEWA JUU YA UNYANYAPAA KWA WAGONGWA WA KIFUA KIKUU

Imetumwa : February 12th, 2025

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS

Jamii imetakiwa kufahamu kwa undani namna ugonjwa wa Kifua Kikuu unavyoenezwa ili kusaidia kuepuka unyanyapaa kwa wagonjwa wa Kifua Kikuu hali ambayo itachagiza mapambano ya kumaliza ugonjwa huo kwa haraka kama malengo ya Serikali yanavyoeleza.

Hayo yameelezwa kwenye kikao kilichowahusisha Maafisa Watendaji wa Kata, Wenyeviti wa Mitaa, viongozi wa madhehebu ya dini na wadau wanaoshirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya Kifua Kikuu kikilenga kuwaelimisha juu ya unyanyapaa kwa wagonjwa katika ukumbi wa ofisi za Zimamoto, Jijini Dodoma leo Februari 12, 2025.

Akielezea umuhimu wa jamii kufahamu hayo, Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Peres Lukango amewaambia viongozi hao kuwa wanatakiwa kuhakikisha jamii wanayoilea kiutawala au kiimani inafahamu Kifua Kikuu, madhara yake na inajua kuhusu unyanyapaa na namna ya kuuepuka.

Kadhalika, Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma kwa Jiji la Dodoma Dr. Rahma Mohamed amesema;

“Leo tumekutana na viongozi hawa ili kuwajengea uwezo na kupata uelewa kuhusu unyanyapaa na waweze kutusaidia kwenye mapambano ya kudhibiti Kifua Kikuu kwani viongozi hawa ndio wanaokutana na jamii kwa ukubwa hivyo watatusaidia kutambua kwa haraka dalili za awali kwa wagonjwa na kutoa taarifa kwenye vituo husika”.

Hatahivyo, Afisa Uhamasishaji na Utetezi Bi. Enel J. Tarimo, kutoka Tanzania TB Community Network (TTCN) ambao ni Mdau anayeshirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya Kifua Kikuu amesema;

“Kifua Kikuu Nchini bado ni janga ambalo linapoteza watu wengi na tunapokea takwimu kubwa kila siku kwa wagonjwa wa Kifua Kikuu na wanaoathirika kuripoti changamoto kubwa ya unyanyapaa kwenye jamii zao hivyo tuliona ni vyema kuwaunganisha wenye jamii wenyewe ili kuielewesha juu ya Kifua Kikuu.”

Haya yote bado ni muendelezo wa Mpango wa kuibua wagonjwa wenye vimelea vya ugonjwa wa Kifua Kikuu kwenye Mkoa wa Dodoma ambapo lengo ni kuibua wagojwa 1,930 ambao hawakuonekana mwaka 2024 ili kufikia malengo ya nchi kumaliza kabisa ugonjwa huo ifikapo 2030.


#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • TAWLA - SAUTI YA WANAWAKE NA WATOTO WALIOKOSA ULINZI WA KISHERIA KATIKA JAMII

    May 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.