• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

HALMASHAURI ZA DODOMA ZATAKIWA KUYAENZI MAENEO YA MICHEZO

Imetumwa : September 20th, 2025

Na. Sizah Kangalawe

Dodoma RS

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amezitaka halmashauri za Mkoa huu kuhakikisha maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya  michezo yanaendelezwa na kutunzwa ipasavyo.

Maagizo hayo yametolewa Septemba 20, 2025 katika Viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma, wakati wa Bonanza la msimu wa pili la Dodoma Fitness lililoandaliwa kwa ushirikiano na Umoja wa 'One Strong Family'.

"Sisi kama Mkoa, katika kuimarisha michezo, tumeendelea kutenga maeneo ya michezo. Na niendelee kuagiza wilaya zote za Mkoa wa Dodoma na maeneo mengine, tuhakikishe maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya michezo yanalindwa, yanatunzwa na yanaheshimiwa bila kuingiliwa, ili kila eneo liweze kufaidika na faida zote za michezo," ameagiza Mhe. Senyamule.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Jabir Shekimweri, amesema bonanza hilo limetumika pia kama fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo mkoani humu.

"Wilaya ya Dodoma kwa kushirikiana na Dodoma 'Fitness Club' tumeona bonanza la mwaka huu lifanyike kwa utofauti. Baada ya kukimbia km 6.8, tutakuwa pia na ratiba ya kufanya utalii wa ndani katika makao makuu ya nchi," amesema Shekimweri.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Dodoma Fitness, Bi. Tatu Rajab, amesema wataendelea kuwa mabalozi wazuri wa vivutio vya utalii mkoani hapo na kwamba bonanza hilo litaendelea kufanyika kila mwaka.

Bonanza hilo limehusisha vikundi mbalimbali vya jogging kutoka mikoa tofauti Nchini kupitia umoja wao ujulikanao kama 'One Strong Family'. Hii ni mara ya pili kufanyika tangu kuanzishwa kwa umoja huo.

Awali, washiriki walikimbia  mbio pole  'jogging' ambazo zilianzia Viwanja vya Jamhuri, kupitia barabara ya Iringa, barabara  ya mzunguko ya Magorofani na kumalizikia tena katika Viwanja vya Jamuhuri, kwa umbali wa kilomita 6.8.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • DODOMA NI SEHEMU NZURI YA UWEKEZAJI

    October 01, 2025
  • CCTV CAMERA KUFICHUA WAVUNJIFU WA SHERIA KATIKA JIJI LA DODOMA

    September 30, 2025
  • DODOMA YAADHIMISHA SIKU YA UTALII DUNIANI KWENYE MICHORO YA MIAMBANI KONDOA

    September 27, 2025
  • JUHUDI KUDHIBITI VIFO VYA WAJAWAZITO ZAPAMBA MOTO

    September 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.