• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KIASI CHA MAFAO YANAYOLIPWA KWA WASTAAFU NI TOSHEREVU - RC SE

Imetumwa : November 11th, 2024

Habari - Dodoma RS

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule ameyasema hayo leo tarehe 12 Oktoba 2024 wakati akifungua semina ya Wastaafu watarajiwa wa Mkoa wa Dodoma.

Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Jijini Dodoma.

Akizungumza na wastaafu watarajiwa Mhe. Senyamule amesema semina hiyo imelenga kuwajengea uwezo na kuwaelekeza wastaafu katika maeneo mbalimbali ikiwemo uwekezaji katika soko la fedha na namna wanavyoweza  kunufaika na mafao ya uzeeni,na kuwa na maisha bora baada ya kustafu.

“Natambua kuwa kulipwa mafao ya uzeeni ni jambo moja na namna ya kutumia mafao ni jambo jingine,dhima  ya hifadhi ya Jamii ni kuwa na raia wenye uchumi imara na endelevu wakati wote”.

“Ni wazi mpango huu ukifanikiwa utajenga msingi imara wa kutumia mafao yanayolipwa na mifuko  ya pensheni kama chanzo cha mitaji ya kutekelezaji miradi mbalimbali midogo midogo na mikubwa.

“ Hivyo kukuza kipato cha Watanzania na kuongeza fursa za ajira hasa kwa vijana wetu na kuna fursa mbali mbali hususani katika kilimo,nyumba za kupangisha na maofisi”Amesema Senyamule.

Hata hivyo Rc Senyamule amewataka wastaafu watarajiwa kutumia mafunzo hayo ili kuepuka matumizi yasiyo na tija ya mafao yanayopelekea mstaafu kuwa na maisha magumu muda mfupi başda ya kupata mafao hayo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF Bw.Abdul-Razaq Badru amesema Mpango huu wa mafunzo kwa Wastaafu watarajiwa wa Mfuko hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuwaanda wanachama wake  wanaokaribia kustaafu waweze kutumia pesa zao vyema katika uwekezaji wenye tija ili kumudu maisha mapya ya ustaafu.

“Wastaafu watarajiwa wanatarajiwa kuwa wamefikiwa baada ya kukamilika kwa semina hii. Mfuko umekuwa na utaratibu wa kutoa elimu kwa wanachama wake wote katika mwaka wa Fedha 2023/2024 jumla ya waajiri 746 kati ya waajiri 981 walifikiwa na tayari katika mwaka huu wa fedha 2024/2025 jumla ya waajiri 207 kati ya waajiri 878 wanatarajia kufikiwa.

Mfuko una jukumu la kuandikisha wanachama, kukusanya michango,  kuwekeza michango maeneo yenye tija na kulipa mafao kwa wanachama.

Mfuko unalipa mafao mbalimbali yaliyoainishwa katika sheria kama vile Mafao ya uzeeni, Mafao ya Ulemavu, Mafao ya kifo, Mafao ya Wategemezi, Mafao ya kukosa ajira, Mafao ya ugonjwa na Mafao ya Uzazi.

Mafao ya uzeeni yanayolipwa kwa wastaafu yakitumika vizuri yanaweza kutoa mchango katika kuendeleza miradi mbalimbali, kutengeneza ajira kwa vijana, kuongeza pato la mstaafu na hatimaye pato la Taifa.  Mfuko tangu kuanzishwa kwake tayari umelipa jumla ya mafao yenye kiasi cha shilingi trilioni 10.46 kwa wanufaika 310,458. 

“Kwa kiasi hiki kilicholipwa ndani ya miaka 6 ya Mfuko, kinaonesha haja ya kuandaa mpango wa mafunzo maalumu kwa ajili ya Wanachama wake wanaotarajia kustaafu ndani ya kipindi cha miaka miwili” Amesema Badru.

Semina hiyo imejumuisha Wastaafu  Watarajiwa kutoka Halmashauri,Wizara,Wakala na Taasisi mbalimbali za Serikali.

&&&

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.