• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

" KILA ANAYEFANYA KAZI DODOMA , AIFAHARISHE DODOMA" RC SENYAMULE

Imetumwa : October 13th, 2022

 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amekutana na kuongea na Viongozi wa Taasisi za Umma zinazopatikana Mkoa wa Dodoma akiwa na malengo makuu matatu ya kujitambulisha, kuonyesha fursa za uwekezaji zinazopatikana kwenye Mkoa pamoja na kujadili namna ya kutunza mazingira.

Kikao hicho kimeanza kwa uwasilishaji wa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Dodoma kwa hadhi ya Makao Makuu  mpango ulioanza mwaka 2019 mpaka sasa, miradi mbalimbali itakayosaidia kukomesha tatizo la upungufu wa maji inayoendelea kama vile ujenzi bwawa la Farkwa, mradi wa kuvuta maji kutoka Bwawa la Mtera na mradi wa kuvuta maji kutoka ziwa Victoria kupitia Singida miradi ambayo bado inaendelea.

Kwa upande wa miundo mbinu ya usafirishaji, kuna mradi wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa Km 213 itakayogharimu kiasi cha Tshs Bilioni 221, uboreshaji wa barabara ya Dodoma – Chamwino unaendelea. Pia ujenzi wa Kiwanja kikubwa cha ndege cha Kimataifa cha Msalato na kuna mpango wa kujenga barabara za mabasi ya mwendo kasi pamoja na usafiri wa reli itakayokua ikizunguka ndani ya Mkoa ikiwa na vituo 28.

Mpango wa uboreshaji wa mazingira pia unaendelea hasa kuifanya Dodoma ya kijani kwa kupanda miti katika maeneo 15 ambayo yameainishwa kwenye mpango yakiwemo Mji wa Serikali Mtumba, pembezoni mwa barabara, mito, vitovu vya huduma, maeneo tengefu kwa kilimo cha Mjini, maeneo ya maziko, viwanda na biashara, maeneo ya wazi n.k

Mkuu wa Mkoa amezitaka Taasisi zote za umma kila mmoja awe mfano kwenye Taasisi yake ili kuleta maana ya kauli mbiu ya Dodoma, fahari ya watanzania.“Neno fahari lina maana nyingi sana na nzito na kubwa zaidi ni lazima uwe zaidi ya wengine. Natoa wito kwenu Taasisi za Serikali kila mtu anayefanya kazi hapa Dodoma, afanye kazi  kwa lengo la  kuifaharisha Dodoma maana ni wajibu wetu na si hiyari kila unachokifanya katika sekta yako, hakikisha kinaupa fahari Mkoa wa Dodoma” Amesisitiza Mhe. Senyamule.

Hali kadhalika, Mhe. Senyamule amewaeleza  wakuu hao maagizo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa Taasisi za Umma.Mhe. Rais amehimiza  pesa inayotengwa kwa ajili ya manunuzi  na ambazo huwa hazitangazwi na  tenda zingine, asilimia 30 ya fedha hizo ziende makundi maalum ambayo ni  ya  wazee 5%, watu wenye ulemavu 5%, vijana, 10% wanawake 10%. Mhe.Rais anatamani watanzania wapate fedha mifukoni. Taasisi za Serikali mnatakiwa kusikiliza kero za wananchi na kuwahudumia. Ningependa Mkoa wa Dodoma tusiwe na kero”

Akizungumzia Mazingira Mhe. Senyamule ameitaka kila Taasisi, ijali mazingira yake kwa kupanda mjiti na kuhakikisha mazingira ya ofisini na hata nyumbani yako safi. Dodoma kuna maeneo ya wazi takribani 160, hivyo utaratibu unafanyijka ili kikla Taasisi ipewe eneo lake na  kulitunza.

Aidha Mkuu nwa Mkoa, ameongeza kuwa Dodoma bado una changamoto nyingi hasa kwenye ufaulu wa wanafunzi. Pamoja na jitihanda za mhe. Rais za kuinua  uchumi wa wananchi , Taasisi zilizopo Dodoma  zinatakiwa  kuangalia na kuja na njia muafaka ya kuona ni kwa namna gani wananchi wananufaika na uwepo wa Taasisi hiyo Mkoani Dodoma .

Mkuiu wa Mkoa, amehitimisha kikao kwa kuwataka Wakuu wa Taasisi kuratibu namna nzuri itakayoweza kusaidia Mkoa wa Dodoma uweze kufikia mipango yote iliyopangwa kwa Mkoa kufikia hadhi yake, kwani uteklezaji wa mpango wa kuifanya Dodoma uwe jiji lenye hadhi ya makao makuu unaenda hadi 2039.Mipango hiyo iwasilishwe ofisini kwake kwani Taasisi zote za umma zilizopo Dodoma zimepata bahati ya kuwa sehemu ya kutimiza  mipango ya Dodoma kwa sasa.

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2020 January 15, 2021
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2020 January 15, 2021
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 SHULE ZA BWENI (WASICHANA NA WANAUME) . December 20, 2020
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA YA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2020 January 15, 2021
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KATIBU TAWALA SINGIDA AKABIDHI OFISI KWA KATIBU TAWALA DODOMA

    March 23, 2023
  • MACHINGA DODOMA WAMPONGEZA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

    March 23, 2023
  • KIWANDA CHA AINA YAKE KUJENGWA KONGWA

    March 17, 2023
  • WAFANYAKAZI WAASWA MSHIKAMANO MAHALA PA KAZI

    March 15, 2023
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Mkoa akiongoza siku ya maombi jijini Dodoma
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.