• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MADEREVA WA SERIKALI WAHIMIZWA KUENDESHA KWA USTADI , KULINDA USALAMA BARABARANI

Imetumwa : September 4th, 2025

Na. Sizah Kangalawe

Habari - Dodoma RS

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amewahimiza madereva wa Serikali kutumia vyema mafunzo waliyopatiwa katika kuboresha utendaji kazi wao na kuleta tija zaidi.

Ameyatoa maagizo hayo Septemba 04, 2025 jijini Dodoma wakati akifunga Kongamano la Nne la Chama cha Madereva wa Serikali Tanzania (CMST) lililofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.

"Naamini mada mlizofundishwa hapa zitakwenda kuboresha uwezo wenu katika utendaji kazi na kuleta tija zaidi katika kuhakikisha mwajiri mkuu ananufaika na mafunzo mliyopata kupitia kongamano hili, na ninaamini kuwa kushiriki kwenu kutapelekea kuendesha magari kwa ustadi na kupunguza matukio ya ajali.

Tutajua thamani ya abiria mliowabeba na kuendesha tukiwa tunawakinga na madhara, lakini pia mtajua thamani ya vitu mnavyobeba kupitia magari hayo ambayo mnatakiwa mvisafirishe kwa usalama," amesema Mhe. Senyamule.

Amefafanua kuwa madereva wa Serikali ni mhimili muhimu katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya Serikali kwani ndio wanaohakikisha usafiri wa viongozi na watumishi unakuwa salama, wenye ufanisi na unaoendana na hadhi ya Taifa la Tanzania.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Dkt. Charles Msonde, amesema Serikali imeboresha muundo mpya wa madereva ambao pia unasimamia maboresho ya mishahara na stahiki nyingine kwa madereva wa Tanzania Bara.

Kongamano hilo lililoandaliwa na CMST, limefanyika kwa siku tano ambapo lilianza Agosti 31 na limetamatika Septemba 04, 2025 huku likienda sambamba na kaulimbiu "Dereva wa Serikali, epuka ajali, linda gari lako na watumiaji wengine wa barabara, shiriki uchaguzi mkuu Oktoba 2025."

Chama cha Madereva wa Serikali kilianzishwa  mwaka 2013 na kusajiliwa Wizara ya Mambo ya Ndani mwaka 2015 kwa Na. ya Usajili S.A. 20314, ambapo hadi sasa kina jumla ya wanachama zaidi ya 3500.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WAHIMIZWA KUENDESHA KWA USTADI , KULINDA USALAMA BARABARANI

    September 04, 2025
  • ACC YATOA VIFAA VYA MILIONI 62 KWA WATOTO WENYE CHANGAMOTO YA AFYA

    September 04, 2025
  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUJIFUNZA TEKNOLOJIA NA MIFUMO YA KISASA YA MAGARI

    September 02, 2025
  • TAASISI ZA KITAFITI TIBA ASILI ZASISITIZWA UFANISI WA VIWANGO VYA KIMATAIFA

    August 29, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.