• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MHE. DKT. CHARLES TIZEBA: WANANCHI MSIUZE CHAKULA GHAFI NJE YA NCHI

Imetumwa : August 5th, 2017

Waziri wa Kilimo, Chakula na Uvuvi Mheshimiwa Dkt. Charles Tizeba amekazia uamuzi wa serikali kuzuia wananchi wasiuze chakula ghafi nje ya nchi ambacho hakijachakatwa na kusagwa kwenye viwanda vyetu, kuwa kusafirisha chakula kwa mfumo huo kunaondosha faida nyingi ambazo zingepatikana ndani ya nchi kama chakula hicho kingesafirishwa kikiwa kimechakatwa na kusagwa viwandani na kufungashwa. Akitaja faida hizo ni kama ajira kwa vijana viwandani, chakula cha mifugo (pumba), malipo au tozo za umeme kwa ajili ya viwanda vyetu na kodi kwa mishahara ya wafanyakazi wa viwanda vyetu ambavyo yote hivyo vinakwenda nje ya nchi yetu endapo tukisafirisha chakula ghafi.

Mheshimiwa Dkt. Tizeba ameyasema hayo Agosti 5, 2017 wakati wa kilele cha Paredi ya Mashindano Maalumu ya saba ya Mifugo ya Kitaifa yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kati vilivyopo Nzuguni nje kidogo ya Mji wa Dodoma ambapo amebainisha kuwa kuchakata chakula na kufungasha pia kuna ongeza thamani kwa wakulima wetu na wafanyabiashara wa chakula tofauti na kuuza mazao yakiwa ghafi. Aidha, ameongeza kuwa Serikali inajitahidi kuendelea kushusha gharama za uzalishaji katika kilimo.

Amesema katika Bunge lililopita Serikali imefuta kodi na tozo zisizopungua 108 zilizokuwa zikisumbua wakulima, wafugaji na wafanyabiashara wengine ambazo zilikuwa kero na ziliongeza gharama ya bidhaa zetu za mazao na chakula na kufanya zishindwe kushindana kwenye masoko Kimataifa kwa kuwa na bei kubwa, lakini pia imeondoa kodi katika mbolea pembejeo na viuatilifu ili kumrahisishia mkulima na sasa serikali iko mbioni hivi karibuni kutangaza bei elekezi kwa mbolea za aina mbili ya kupandia aina DAP na kukuzia aina ya UREA.

Nae Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Nane Nane Kanda ya Kati Bi. Aziza Mumba alibainisha kuwa mwaka huu 2017 yanafanyika Maonesho ya kumi (10) katika uwanja wa Nzuguni. Kwa upande wa mifugo yanafanyika Maonesho ya saba (7) Kitaifa kuanzia mwaka 2011. Uwanja wa Nzuguni ni kituo cha kudumu kwa Maonesho ya mifugo Kitaifa. Amesema kwa miaka yote 8 ya nyuma, kulikuwa na mahudhurio makubwa ya watazamaji na waoneshaji.

Ametaja Kaulimbiu ya mwaka huu 2017 ni “ZALISHA KWA TIJA MAZAO NA BIDHAA ZA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI ILI KUFIKIA UCHUI WA KATI” akihusisha na Malengo ya Maonesho ya Mwaka huu kuwa ni utoaji wa elimu ya matumizi ya teknolojia mbalimbali kwa wadau wengi kwa muda mfupi. Wadau watajifunza kwa njia ya kuona, kujadiliana na kuulizana maswali. Maeneo makuu ya mafunzo ni teknolojia za uzalishaji wenye tija wa mazao, mifugo na usindikaji wa bidhaa kuongeza thamani. Teknolojia nyingine zitakazooneshwa ni hifadhi ya mazingira, vyanzo vya nishati mbadala, zana na pembejeo bora za kilimo na mifugo zipatikanazo nchini na teknolojia za mawasiliano.

Ameongeza kuwa Wadau pia watajionea na kujifunza huduma zitolewazo na Serikali, Mashirika ya umma na binafsi, Aidha Maonesho hutumiwa na wafanyabiashara kuuza bidhaa, kufahamiana na kuingia makubaliano. Halikadhalika, watu wamekuwa wakipata fursa ya kuwaona baadhi ya wanyamapori katika Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.