• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MHE.RAIS ANALETA SHULE ILI WATOTO WASITEMBEE UMBALI MREFU ; RC SENYAMULE

Imetumwa : December 13th, 2024

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS

Ikiwa ni siku chache zimesalia kuanza muhula mpya wa masomo Nchini mnamo Januari 13, 2025, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amefanya ziara ya kikazi kutembelea miradi ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kata ya Matumbulu pamoja na ujenzi wa madarasa katika shule ya Sekondari Kata ya Miyuji B zote za Jijini Dodoma.

 Ziara hiyo imelenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule na madarasa hayo ili kujihakikishia kuwa wanafunzi wote waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza 2025, wataweza kuanza masomo yao bila adha ya kutembea umbali mrefu pamoja na kupunguza msongamano madarasani.

“Matamanio ya Rais kuleta hizi shule ni ili watoto wasitembee mwendo mrefu kwenda shule, bado tuna changamoto ya utoro inayochangiwa na watoto kutembea mwendo mrefu lakini pia tuna ukatili wa kijinsia ambao hufanyika watoto wakiwa wanaelekea shuleni, yote haya Mhe. Rais ametaka ayamalize kwa kuwajengea shule karibu na maeneo yao” Amesema Mhe. Senyamule.

Aidha, Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma Bi. Sakina Mbugi, amesema kuwa, Mhe. Rais ametoa fedha ili kuboresha mazingira ya kujifunza na kujifunzia kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma ili kupigana na adui ujinga hivyo, wao kama Wataalamu wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati uliokusudiwa.

Mradi wa Shule mpya ya Sekondari Kata ya Matumbulu ulitengewa kiasi cha shilingi 544,225,526 kwa ujenzi wa madarasa 8, ofisi 2, jengo la Utawala, maabara za Fizikia, Baiolojia na Kemia, jengo la TEHAMA, choo, kichomea taka na tanki la maji la ardhini. Ujenzi umefikia hatua ya pili ya kuezeka.

Katika shule ya Sekondari Kata ya Miyuji B inayotekeleza mradi wa ujenzi wa miundombinu ya nyumba 2 za walimu, mabweni 2, matundu 10 ya vyoo na madarasa 4 kwa kiasi cha shilingi 454,000,000 kutoka katika mradi wa SEQUIP unaohusika na kuboresha miundombinu ya elimu, umefikia hatua ya kuezeka ambapo miradi yote hiyo inatarajiwa kukamilika Disemba 30, 2024.


#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu                              

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.