• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC AKUTANA NA KUFANAYA KIKAOA NA WAENDESHA BODABODA NA BAJAJI JIJINI DODOMA

Imetumwa : May 24th, 2022


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka, Mei 24, 2022 kwenye ukumbi wa Cavillum alikutana na kuongea na madereva wa Pikipiki maarufu kama Bodaboda pamoja na Bajaji kuzungumzia utendaji kazi wao, hali ya ulinzi na usalama kutokana na matukio ya kihalifu yanayofanywa na baadhi yao pamoja na changamoto wanazokumbana nazo wakati wa usafirishaji wa abiria.

Katika kikao hicho, Mhe. Mtaka aliongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, wakuu wa idara zinazohusika na usafirishaji kama vile Wakala wa barabara za vijijini TARURA, Mamlaka inayoshughulikia usafirishaji wa nchi kavu LATRA , Mkuu wa kitengo cha Usalama barabarani pamoja na wadau wanaoisaidia kuiwezesha sekta ya usafirishaji kifedha ambao ni Benki ya NMB pamoja na shirika la Bima la SANLAM.

Baadhi ya madereva wa vyombo hivyo, walitoa malalamiko yao mbele ya Mkuu wa Mkoa kwamba wananyanyaswa na vyombo vinavyohusika na usalama barabarani kwa kulipishwa faini zisizo na risiti, kubabimbikiwa makosa ambayo wakati mwingine hayahusiani na usalama barabarani.

Akijibu tuhuma hizo, Meneja wa TARURA Mkoa wa Dodoma Bwana Lusako Kilembe, amesema kuwa sheria ya ulipaji faini za barabarani unafanyika kwa kutumia namba maalumu za malipo zinazojulikana kama Control number na si vinginevyo hivyo ametoa wito kwa madereva hao kutokubali kufanya malipo kwa afisa yeyote wa TARURA kwa kumpatia fedha mkononi

Pia Bwana Kilembe ameongeza kuwa wapo kwenye mchakato wa kubadilisha mamlaka itakayohusika na upokeaji wa faini za barabarani ambapo Halmashauri ya Jiji ndio itahusika kwa hilo na si TARURA tena.

Kwa upande wa Mamlaka ya usafirishaji nchi kavu LATRA ambayo pia ilielekezewa malalamiko na madereva hao, Bwana EzekieI Emmanuel, Afisa mfawidhi wa Mamlaka hiyo Dodoma, amejibu baadhi ya tuhuma ikiwemo suala la kukamata pikipiki ikiwa nje ya kituo ambapo alisema vyombo hivyo vinatakiwa kuwa na usajili na kukaa kwenye vituo vyao kusubiri abiria kwani hii itasaidia kupunguza uhalifu.

Aidha, ameongeza kuwa, gharama ya kulipia leseni kwa pikipiki kwa mwaka ni shilingi 17,000/-, na kwa bajaji ni shilingi 20,000/- hivyo endapo malipo yatachelewa, huwa kuna faini ya ongezeko la shilingi 10,000 ambapo amewataka madereva hao kutii sheria bila shuruti na kuzingatia muda wa ulipiaji wa leseni zao ili kuepuka faini hizo.

RC Mtaka alihitimisha kikao hicho kwa kutoa neno kwa madereva hao kwa kuwaasa kuiheshimu kazi yao na kuitaka Mamlaka husika kuiangalia kwa karibu sheria ya uvaaji wa kofia ngumu kwa abiria wa pikipiki kwani kulingana na hali iliyopo ya mlipuko wa ugonjwa wa Uviko 19, uchangiaji wa kofia hizo unaweza kuongeza maambukizi zaidi.

Amewaasa bodaboda kukerwa na matukio ya uvunjifu wa amani yanayoendelea kufanywa kwa kutumia pikipiki miongoni mwa wenzao wasio waaminifu. Pia amesema lengo la Mkoa ni kutengeneza kundi jipya la wafanyabiashara miongoni mwa pikipiki kwani zitakaposajiliwa itakua rahisi kupata mtandao mkubwa wa abiria na amewataka kuacha mara moja kujichukulia sheria mikononi pindi inapotokea ajali inayohusisha bodaboda.

Mhe.Mtaka amezisihi mamlaka husika kwa kushirikiana na madereva hao kuhakikisha wanakomesha suala la rushwa na kila dereva ajisajili kwenye mifuko ya penseni kama NSSF, iCHF, NHIF kwani itawapunguzia gharama za matibabu na kupata mafao ya uzeeni pindi atakaposhindwa kuendelea na kazi au kustaafu. Mwisho.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.