• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC MTAKA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAFANYABIASHARA WAKUBWA MKOANI DODOMA

Imetumwa : June 18th, 2021

HABARI PICHA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Wafanyabiashara Wakubwa Mkoani Dodoma.

Baadhi ya Wafanyabiashara Wakubwa wa Mkoa wa Dodoma wakiwa kwenye kikao na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka

Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Dodoma Ndg. Deus Nyabiri akichangia hoja kwenye mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Wafanyabiashara wakubwa Mkoani Dodoma.

................................................................................................................................................................


RC MTAKA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAFANYABIASHARA WAKUBWA MKOANI DODOMA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka, leo Juni 18, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Wafanyabiashara wakubwa Mkoani Dodoma kwa lengo la kupokea maoni yao kuhusu Mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji katika Mkoa wa Dodoma.


Kikao hicho kilichofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, kimewajumuisha Wafanyabiashara wakubwa kutoka sekta mbalimbali, wakuu wa Taasisi zinazotoa huduma na zinazosimamia masuala ya biashara na uwekezaji zikiwemo Idara ya Kazi, Wakala wa Vipimo, TANESCO, TARURA, DUWASA, TIC, TRA, TBS, OSHA, TMDA na Viongozi wa Halmashauri ya jiji la Dodoma. 


Mhe. Mtaka amewaeleza wafanyabiashara kuwa yeye ni muumini Mkubwa wa Sekta Binafsi kwa kutambua ukweli kuwa ndio wachavushaji wa uchumi kukua na kwamba licha ya Serikali kuwa Muajiri Mkuu, Sekta Binafsi imeendelea kuwa muajiri wa wakati wote huku ikiwa na fursa lukuki za kufanya uchumi na uzalishaji.

“Tukitaka jiji la Dodoma liwe shindani ndani na nje ya jumuiya ya Afrika Mashariki, liweze kushindana na majiji kama Nairobi, Kampala, Bujumbura, Kigali na Majiji mengine makubwa nje ya Afrika, lazima Sekta Binafsi ijipambanue na kustawisha shughuli zake na katika kipindi cha uongozi wangu kama Mkuu wa Mkoa wa Dodoma nitahakikisha Serikali inailinda Sekta Binafsi” alibainisha Mhe. Mtaka.


Aliwataka Wadau wa Sekta Binafsi katika Mkoa wa Dodoma kujipanga vema ili kuweza kufaidika na fursa za kuwekeza zinazotokana na Serikali kuhamishia shughuli zake Makao Makuu ya Nchi na hata wanapokuja Wawekezaji wakubwa kutoka Nje ya Nchi, Sekta Binafsi waweze kuingia nao mashirikiano katika uwekezaji mbalimbali. 


Nae Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara, Wakulima na Wenye Viwanda Mkoa wa Dodoma – TCCIA Ndg. Deus Nyabiri ameitaka serikali kupitia Mamlaka ya Mapato TRA kuhakikisha inaongeza program za utoaji elimu ya kodi na kuhakikisha inawafikia Wafanyabiashara wote kuanzia Wakubwa hadi wajasiriamali wadogo ili wawe na utamaduni wa kulipa kodi wao wenmyewe bila kushurutishwa.


Aidha, ameitaka Halmashauri ya Jiji la Dodoma kushindana na majiji mengine makubwa ndani na nje ya Afrika kwa kuboresha  miundombinu ya maeneo ya kufanyia biashara kama vile masoko, vituo vya mabasi na kuweka mifumo rafiki ya uendeshaji ambayo haitageuka kero kwa wananchi wanaotegemea huduma hizo.


Ametoa Rai kwa Uongozi wa Mkoa wa Dodoma kuhakikisha inahuisha mabaraza ya biashara ya Mkoa na Wilaya na Majukwaa ya Kodi ili yafanye kazi yake ya msingi ya kuwa majukwaa ya majadiliano kati ya wafanyabiashara/wawekezaji na serikali na taasisi zake ili kuendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji katika Mkoa wa Dodoma.


Kwa upande wake Mjumbe wa TCCIA Taifa Ndg. Faustine Mwakalinga amezitaka Taasisi mbalimbali za Serikali zinazosimamia shughuli za biashara na uwekezaji kufanya kazi kwa ushirikiano kama timu mmoja ili kuondoa urasimu, usumbufu na ucheleweshaji wa utekelezaji miradi kwa kuchelewesha au kukwamisha vibali mbalimbali.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.