• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Vijana Waliofadhiliwa na Serikali kwenye vyuo Vua Fundi,Wametakiwa Kuwa Waadilifu, Wenye Nidhamu na Kujituma

Imetumwa : July 19th, 2022

WANAFUNZI wanaosomea ufundi katika vyuo vya ufundi vilivyopata ufadhili wa Serikali wametakiwa kuwa waadilifu katika katika kazi zao pindi watakapomaliza mafunzo yao na kuanza kazi kwani hiyo itafanya waaminike kwa wateja wao na hivyo kukuza biashara zao.

Ushauri huo umetolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako wakati akizungumza na wanafunzi wa vyuo ya ufundi vya Donbosco na Veta vya jijini Dodoma Kwenye ziara hiyo Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amejionea jinsi wanafunzi wa kike na wakiume wakijifunza mafunzo mbalimbali yakiwemo Mapishi, mapambo, kuchomelea na kuunga vyuma, uselemala utengenezaji wa magari na kilimo ambapo amewapongeza wanafunzi kwa kuonyesha bidii ya kujifunza.

Waziri Ndalichako amesema kuwa vijana hao mara baada ya kumaliza kozi zao za mafunzo ya miezi sita watakuwa wamejifunza kutengeneza mazingira mazuri ambayo yatawawezesha kuaminika katika kazi zao badala ya kujiingiza  kwenye vitendo vya Udokozi kama ilivyo kwa baadhi ya mafundi wa fani mbalimbali waliopo mitaani.“Mkienda mitaani kaanzisheni kazi zinazotokana na fani hii ya ufundi mtakayoipata chuoni lakini msifanane na wale wengine ambao ni wadokozi wa vifaa vya watu vya ujenzi au chochote kinachohusisha ufundi wao. Tuwe na nidhamu, tujitume, tuwe wenye uadilifu katika kazi tutakazopata, tusibaki kulalamika badala yake tutengeneze mazingira ya kutegemewa na kuaminika na wateja badala ya kugeuka kuwa mizigo kwao na kwa Serikali”.

Aidha Waziri Prof. Ndalichako amewaleza wnafunzi hao kuwaa anatekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri Ya muungano Wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan hivyo wasimuangushe wasome kwa bidii na kile wanachokipata wakakifanyie kazi sawa na malengo ya Serikali.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amewataka  vijana hao kuwa kama vinyozi ambao wao hawawezi kuondoka na  kichwa cha mtu “msiwe wababaishaji mkawe waamifu msidokoe vipuri vya watu”. Amesisitiza Mhe. Mtaka

Nae, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Jabir Shekimweri amesema malengo ya zile asilimia 10 za wanawake, vijana na kwa wenye ulemavu hapo ndiyo sehemu sahihi “mikopo hii ya asilimia 10 hapa ndiyo mahala pake hivyo wale ambao  wataingia 10 bora katika ufaulu watapewa mikopo ya kujiendeleza hivyo kazeni buti katika kujifunza”. Amesema Shekimweli.

Kwa upande wake mkuu wa chuo cha Donbosco Padri Bonface Mchome amesema chuo chake kimepokea vijana 276 ambao wamefadhiliwa na Serikali ya Tanzania.Aidha kwa upande wa Chuo cha VETA Mkuu wa Chuo hicho Bw. Stanslaus Ntibara amesema wao wamepokea 351 na kwamba walioripoti mpaka sasa ni 29.

Akizungumza Mwanafunzi wa ufundi Bomba wa Chuo cha VETA, Wambi Mwakifula amesema anafikiria yeye akishamaliza masomo yake ya ufundi stadi atakuwa wakala wa mafundi ambapo atanunua vifaa vyakutosha ambavyo vitawezesha mafundi wengine kufanyia kazi.“Jana nilikuwa nafikiria kuwa uwakala wa ufundi ni mzuri nitakuwa nanunua vifaa vya kutosha vya ufundi kisha nawakusanya mafundi kwenye ofisi yangu ambayo itakuwa ikipokea kazi na kuwapa mafundi kwenda kufanya huku ofisi ikipatana na mteja badala ya wao kupatana na wateja moja kwa moja, naona itakuwa njia nzuri ya kujipatia kipato”. Amesema Wambi Mwakifula.

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.