• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

VITUO VYA AFYA MSINGI MKOANI DODOMA VYAONGOZA MATUMIZI YA MFUMO WA ‘ GoTHOMIS’ KWA 98%

Imetumwa : June 12th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Mkoa wa Dodoma unatajwa kuongoza kwa asilimia 98 ya matumizi ya Mfumo wa Serikali wa utoaji huduma za Afya (GoTHOMIS) kwenye vituo vyote vya afya msingi vilivyosimikwa Mfumo huo kwa ufadhili wa Shirika la KOICA kutoka Serikali ya Muungano wa Korea kwa ushirikiano na Serikali ya Muungano wa Tanzania.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI – anayeshughulikia masuala ya Afya Prof. Tumaini Nagu wakati akifungua kikao kazi cha tathmini ya Matumizi ya Mfumo huo katika vituo vya afya vya Mkoa wa Dodoma kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo leo Juni 12, 2025.

“Kwa ujumla 78% ya vituo vya afya msingi vimefanikiwa kusimika na kutumia Mfumo huu. Hii ni kwa wastani, lakini tukiongelea mikoa mingine ambayo ipo nyuma kama Mkoa wa Pwani wanakaribia 60% lakini wanavutwa na Mkoa wa Dodoma ambao sasa unasimamia kwenye 98%, haya ni mafanikio makubwa”.

Aidha, Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya Dr. Gidion Mnzava amesema kupitia msaada wa KOICA, vituo vya afya 235 vimesimikwa Mfumo huo ambao unarahisisha usajili, utunzaji rekodi sambamba na uwasilishaji wake wenye ubora kwa njia ya kidijitali pia mafunzo yanayotolewa kwa watumishi juu ya matumizi ya vifaa, yamechangia kwenye utoaji wa huduma bora za afya.

Kwa upande wake, Makamu Mkurugenzi Mkaazi wa KOICA nchini Tanzania Bw. Seunghoon Beck, amewataka wadau walioahidi kukamilisha usimikaji wa vifaa vya Mfumo huo kwenye vituo vilivyosalia, kuhakikisha wanakamilisha kabla ya muda wa mradi kuisha ili huduma za afya ziweze kutolewa kwa njia za kisasa kwa kuwa Serikali yake itaendelea kudumisha ushirikiano mzuri uliopo baina ya nchi hizi mbili.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya, amesema Dodoma inafanya vizuri kwenye matumizi ya GoTHOMIS hivyo, kazi iliyobaki ni kwa Wakurugenzi wa Halmashauri kuunganisha Mfumo huo na ule wa Serikali ili kuboresha ufuatiliaji wa karibu kwenye ukusanyaji wa mapato kutoka katika vituo vya afya lakini pia kuweka rekodi zilizo bora.

Mradi wa usimikaji vifaa, mafunzo na matumizi ya Mfumo wa GoTHOMIS kwenye vituo vya afya unaotekelezwa na Shirika la KOICA nchini Tanzania, ulianza 2021 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba 2025, unatajwa kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya hivyo kupunguza changamoto mbalimbali ikiwemo upotevu wa taarifa za wagonjwa.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA YAPONGEZWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA 2023/2024

    June 13, 2025
  • KIWANDA CHA NONDO KINACHOTUMIA UMEME JUA KUJENGWA CHAMWINO MKOANI DODOMA

    June 13, 2025
  • RAIS DKT. SAMIA KUFANYA ZIARA JIJINI DODOMA

    June 13, 2025
  • DODOMA YAENDELEA NA MAANDALIZI KUELEKEA SIKU YA KUPINGA DAWA YA KULEVYA DUNIANI

    June 12, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.