• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

NGO’s DODOMA ZATAKIWA KUWAJIBIKA KWA SHERIA NA TARATIBU

Imetumwa : July 23rd, 2025

Na. Sizah Kangalawe – Habari, Dodoma RS

Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) yanayotekeleza shughuli zake mkoani Dodoma yametakiwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji ili kuhakikisha yanatoa mchango chanya kwa maendeleo ya jamii bila kukiuka misingi ya utawala bora. Wito huo umetolewa katika mkutano wa mashirika hayo, uliofanyika Jijini Dodoma Julai 23, 2025.

Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala Msaidizi, Seksheni ya Viwanda na Uwekezaji, Bi. Mwajabu Nyamkomola, alipomuwakilisha RC Rosemary Senyamule katika ufunguzi wa mkutano wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Dear Mama jijini Dodoma.

"Ofisi ya Mkuu wa Mkoa isingependa kupokea malalamiko ya ukiukwaji wa sheria na kanuni unaofanywa na baadhi ya mashirika, badala ya kuhakikisha jamii inapata maendeleo yaliyokusudiwa.

"Nitumie fursa hii kuwakumbusha wote kuwa makini, kuongeza ufanisi na kuepuka migogoro ya aina yoyote ili kuleta maendeleo yaliyokusudiwa."

Hata hivyo, Bi. Nyamkomola ameyataka mashirika hayo kufanya kazi zao kwa uwazi hususan katika vyanzo vyao vya mapato.

"Ninaamini kupitia mkutano huu, tutaweka makubaliano ya utekelezaji wa pamoja na uwazi katika vyanzo vya mapato, aina ya miradi, maudhui ya miradi, na uwajibikaji kwenye mipango yote inayotekelezwa kuanzia ngazi ya vijiji, kata, wilaya hadi mkoa ili kurahisisha kazi ya usimamizi na ufuatiliaji," amesema Nyamkomola.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NACONGO) Mkoa wa Dodoma, Bw. Isaya Silungwe, ameweka bayana mwelekeo wa Taasisi hizo kwa miaka mitano ijayo.

"Mashirika Mkoani Dodoma yameweka vipaumbele ikiwa ni pamoja na kuimarisha mifumo ya kiutawala, uwazi na uwajibikaji, kuanzisha miradi ya uzalishaji mali ili kupunguza utegemezi wa wafadhili, pamoja na kuanzisha mfuko wa maendeleo wa kusaidia mashirika yenye changamoto," amebainisha Silungwe.

Naye Msajili wa mashirika hayo Mkoa wa Dodoma, Bi. Honoratha Rwegasira, amesema mkutano huo wa siku mbili, ukijumuisha ushiriki wa mashirika 211, umefanyika kwa ngazi ya mkoa ambapo awali ulitanguliwa na mikutano ya ngazi za wilaya ikiwa ni kuelekea mkutano wa ngazi ya Kitaifa unaotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.


#DodomaFahariYaWatanzania

#KeroYakoWajibuWangu

#TakeDodomaToTheWorldAndBringTheWorldToDodoma

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • VIJANA RIKA BALEHE 13,218 MKOA WA DODOMA WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA MRADI WA AHADI

    July 23, 2025
  • MAAMBUKI YA UGONJWA WA HOMA YA INI ‘B’ YAFIKA 3.5% KITAIFA

    July 24, 2025
  • DODOMA NBC MARATHON YALENGA KUOKOA MAISHA YA MAMA NA MTOTO

    July 24, 2025
  • NGO’s DODOMA ZATAKIWA KUWAJIBIKA KWA SHERIA NA TARATIBU

    July 23, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.