• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WANAWAKE CHANGAMKIENI FURSA - SENYAMULE

Imetumwa : March 12th, 2023

Wanawake wametakiwa kujipambanua na kuchangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza na kuthubutu kuzifanya kwa juhudi na maarifa ili kuepuka utegemeze kwa kila kitu.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Dodoma mhe. Rosemary Senyamule alipozungumza na wanawake wa Mkoa wa Dodoma na viunga vyake katika ukumbi wa “Dear Mama” hotel jijini Dodoma katika hafla ya mwanamke mwamba iliyoandaliwa na Cfm redio na kuhudhuriwa na wanawake wa makampuni mbalimbali.

"Hafla kama hizi zinapendeza pia kuwapa taarifa kuwa Serikali inatambua uwepo wenu na tunafanya kazi na wanawake pia, ukisikia kuna zabuni zimetangazwa na serikali changamkieni na tafuta timu yako mkafanye kazi, hata ukishika zabuni ya kuleta tofali tuu ili mradi kwenye zile 10% za ushiriki hata kwa 3% acheni kuogopa jaribuni mnaweza” Amesisitiza Mhe. Senyamule.

"Niwaongeze Cfm kwa kutambua na kuona umuhimu wa kumpa motisha mwanamke mpambanaji nimesikia redio yenu imeanzishwa juzi tu mwaka 2020 lakini mpaka sasa mmshatoa tuzo miaka mitatu mfululizo hii inamaanisha mnathamini juhudi za wanawake wa Dodoma, niwatie moyo endeleni hivi hivi mnawapa nguvu ya kuthubutu na wale waliolala kuamka na kufanya kazi" Mhe. Senyamule amebainisha.

Nae Mkuu wa Ubunifu wa Cfm redio Samwel Andrew amesema ni wakati wa wanawake kuanza kujitegemea na kufanya kazi kwa bidii ili kuienzi dhamira kuu ya kuadhimisha hafla ya mwanamke mwamba ya kutoa fursa kwa mwanamke wa Dodoma na Kanda ya kati kutambua thamani yake katika jamii.

"Ni wakati sasa wanawake kuanza kujitegemea na kuanza kufanya kazi kwa bidii ndani ya familia, hapa ni kuangazia wajibu wa mwanamke katika familia na hata jamii husika, kuhakikisha kila fursa inayotokea mwanamke asibaki nyuma na kuanza kumtegemea mwanaume kuwa atafanya, baadhi ya wanawake wamekuwa wakitegea kuwa ni lazima mwanaume awajibike kwa kila nafasi lakini si wanaume wote watakuwa na mtazamo wa kuwajibika vyema.

"Ni wakati wa wanawake wote kusema wanaweza, hii italeta mawazo chanya na mtazamo mzuri katika jamii na kuleta ushawishi mkubwa wa jamii kuanza kuamini kuwa pia hata wanawake wanaweza kuleta mabadiliko makubwa, kwa namna hii wanawake wengi watajua wajibu wao katika jamii na kuanza kuzijua fursa nyingi ndani na nje ya nchi", Amesema Bw. Andrew

Aidha katika hafla hiyo Cfm kupitia tuzo ya mwanamke mwamba wa kusaidiwa kwa kushirikiana na wadau wengine wamemkabidhi Bi. Beatrice Makenga (mlemavu wa miguu) mtaji wa friji ili aweze kufanya biashara ya kuuza 'barafu’ ambayo itamsaidia kujikimu kimaisha na familia yake pia Beatrice alikabidhiwa zawadi mbalimbali kutoka kwa wanawake miamba waliohudhuria hafla hiyo.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.