Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Tume ya Takwimu imefanya Kongamano kubwa la kuwajengea uwezo na kuwapa ujasiri watu wenye ulemavu kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la Sensa linalotarajiwa kufanyika nchini Agosti 23. Kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa JKCC Jijini Dodoma huku mgeni rasmi akiwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ambaye amewakilishwa na Waziri wa nchi, Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene (Mb).
Akitoa maelezo mafupi kuhusu zoezi la Sensa, Mkurugenzi wa Tume ya Takwimu Nchini (NBS) Dkt. Albina Chuwa, amesema Sensa ya mwisho iliyofanyika nchini mwaka 2012, ilipata idadi ya watu Mil 34.3 huku watu wenye ulemavu wakiwa asilimia 2,hii ni kutokana na ukosefu wa uhamasishaji kwa kundi hili maalumu katika Jamii kwani halikushirikishwa vyema pia maswali yaliyoulizwa kuhusu walemavu yalikuwa mawili tu.
Sanjali na hayo "Sensa ya mwaka huu 2022 inatarajiwa kufikia idadi kubwa zaidi ya kundi hili na kwenye dodoso la Makarani wa Sensa kutakua na maswali zaidi ya 10 yatakayohusu watu wenye ulemavu ". Amesema Dkt. Chuwa.
Mwenyekiti wa Walemavu nchini Bw. Diwani Kimaya amesema Kongamano hili ni Utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais juu ya ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu kwenye zoezi la sensa ya watu na makazi mwaka 2022.
"Kongamano hili lina dhumuni la kufungua ufahamu kwa kundi hili kupata kuhamasisha na wengine wasio na mwamko waweze kujitokeza kuhesabiwa". Amesisitiza Bw.Kimaya.
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu - Mhe.Ummy Ndeliananga ametoa pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kulivalia njuga suala la Watu wenye Ulemavu, aiha Mhe. Ndeliananga amemshukuru Mhe. Ras kwa kumwamini ābungeni tupo wabunge 8 wenye ulemavu. Wote kwa pamoja tunajenga na kutetea ajenda zenu kwa ukubwa. Jumuiya Bendi hongera sana kwa kazi nzuri name ni mlezi wa bendi hiyo. Ili kuibua vipaji mbalimbali vya watu wenye ulemavu napendekeza kuwe na Bonanza la watu wenye ulemavu,kwani kupitia Bonanza hilo tunaweza kuibua vipaji maalum ya watu wenye ulemavu.
Naibu Waziri wa Ajira, vijana na watu wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi, ameongelea vipaumbele sita vya Mhe. Rais Samia kwa watu wenye ulemavu kuwa ni kusimamia haki za kibinadamu kwa watu wenye ulemavu na watakaokiuka hatua kali za kisheria zitachukuliwa. Watu wenye ulemavu washirikishwe kwenye eneo la uchumi yaani kilimo, mikopo na mabenki. Ajira ambapo asilimia 3 ya nafasi za ajira iwe ni kwa ajili ya watu wenye ulemavu.Elimu jumuishi katika zote, Mhe. Rais Samia Suluhu tayari amewezesha upatikanaji wa mabweni 50 katika halmashauri 50 yote hayo yatatumiwa na watu wenye ulemavu . Aidha Mhe. Rais tayari ametoa zaidi ya Tsh.3bln kwa ajili ya kuboresha vyuo vya walemavu.
Mhe Katambi ameongeza kuwa, Rais ametoa 3.0 bln kwa ajili ya kuboresha Vyuo vya Ufundi vya watu wenye ulemavu vilivyokufa katika mikoa ya Tabora, Singida, Mwanza na Tanga na fedha nyingine imetolewa kwa ajili ya uzalishaji wa Mafuta ya wenye ulemavu wa ngozi katika hospital ya KCMC. Aidha Mhe. Rais, ametoa kiwanja Na. 162 block AL kilichopo Mtumbwa Kwa ajili ya shirikisho la watu wenye ulemavu kiwanja hicho kina thamani ya Tsh. 36.0 mln. Pia Mhe. Rais ametoa kiasi cha Tsh. 300.00 ml kwa ajili ya mapitio ya sera ya walemavu.
Akizungumza kwa niaba ya Mgeni rasmi, Mhe Simbachawene, amesema, Taifa litapiga hatua kubwa kimaendeleo tukipata takwimu sahihi za watu wenye ulemavu kupitia ushirikishwaji wao, utasaidia sana kwenye utungaji wa sera zenye kutetea maslahi yao.
Aidha Mhe. Simbachawene amewaagiza Ofisi ya Takwimu ya Tanzania Bara pamoja na Zanzibar kuendelea kuboresha taarifa za upatikanaji wa taarifa za idadi ya watu na kuwe na mfumo ambao utatusaidia kupata taarifa hizo kabla ya sensa ijayo."Ofisi za takwimu muendelee na uboreshaji wa uhifadhi wa takwimu za walemavu na hakikisheni Kamati za watu wenye ulemavu zinashirikishwa kwa kiwango cha kutosha katika hatua zote za awali mpaka hitimisho la siku ya sensa yenyewe Agosti 23". Amesisitiza Mhe. Simbachawene.
MWISHO
Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa
Anuani ya Posta: 914 DODOMA
Simu: +255 26 232 4343/232
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz
Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.