• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WATUMISHI HODARI 2025 KUTOKA OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA WAPONGEZWA

Imetumwa : May 9th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Watumishi Hodari kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, wamepongezwa kwa kujitoa na kujituma kufanikisha shughuli mbalimbali za Mkoa huu hali iliyosababisha wachaguliwe kuwawakilisha wengine kwenye zawadi za wafanyakazi hodari wakati wa sherehe za Mei Mosi 2025 zilizofanyika Kitaifa Mkoani Singida.

Pongezi hizo zimetolewa Mei 09, 2025 na Mkuu wa Mkoa huyo Mhe. Rosemary Senyamule alipozungumza kwa njia ya simu na Watumishi hao kwenye hafla fupi ya chakula cha pamoja iliyoambatana na kuwapongeza Watumishi Hodari akiwemo Mtumishi Hodari  wa jumla Mhandisi David Chitemo.

“Tumezifanya shughuli zile kwa ushirikiano mkubwa na najua watumishi walikua tayari. Pia nawapongeza wale wenzetu waliotuwakilisha kwa kupata zawadi za kuwa wafanyakazi hodari,ambapo pamoja na zawadi zile, niliagiza leo tufanye shughuli maalum ya kuwapongeza na kuwakabidhi zawadi zetu.” Mhe. Senyamule.

Aidha, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya ametumia jukwaa hilo kuwahimiza Watumishi wake kuwekeza kwenye kilimo cha matunda ya Matufaha ‘Apples’ ambacho kinaonekana kitafanya vizuri katika Mkoa wa Dodoma na soko lake ni kubwa.

“Uzuri wa ‘apples’, baada ya kuvuna inaanza tena, yaani inazaa ‘continuously’. Mkuu wa Mkoa alikwenda akapiga picha, tumeona ‘apples’ ambazo zilivunwa na ukiziona huwezi kuamini kama ni za Dodoma, unaweza kufikiri zimetoka South Afrika. Sasa tunakwenda kuhamasisha hili jambo na tunasikia zinapatikana Iringa, na mche ni shilingi 12,000 tu”.

Akitaja vigezo na sifa za kuchaguliwa kuwa Mfanyakazi hodari wa mwaka, Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Utawala na Usimamizi wa  Rasilimali watu Mkoa wa Dodoma Bi. Coletha Kiwale;

“Baadhi ya vigezo vya kupata Mfanyakazi hodari ni yule ambaye sio malalamishi, anayeweza kupokea ushauri kutoka kwa Watumishi wengine, Mfanyakazi ambaye ni mbunifu lakini ambaye pia anatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu lakini pia anaweza kupokea ushauri kutoka kwa Watumishi wengine.”

Watumishi Hodari 2025 waliopongezwa ni Mhandisi David Chitemo (Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji), Bi. Grace Moshi (Kitengo cha TEHAMA), Bi. Vaileth Nanyaro (Seksheni ya Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi), Bw. Jacob Mang’ombe (Seksheni ya Utumishi), Bw. Moses Kawage (Ukaguzi wa ndani), Bi. Salma Kilili (Seksheni ya Elimu), Dr. Peres Lukango (Seksheni ya Afya) na Mhandisi Ismail Kilima (Seksheni ya Miundombinu).


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI HODARI 2025 KUTOKA OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA WAPONGEZWA

    May 09, 2025
  • MRADI WA KUIMARISHA HUDUMA ZA KIFAFA WAZINDULIWA DODOMA

    May 08, 2025
  • UBALOZI WA UINGEREZA NCHINI TANZANIA WAADHIMISHA MAFANIKIO YA MWAKA MMOJA NCHINI

    May 08, 2025
  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.