• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WEZI WA MIUNDOMBINU YA SERIKALI KUSHTAKIWA KAMA WAHUJUMU UCHUMI

Imetumwa : September 19th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ametoa onyo kwa wananchi wasio waaminifu wanaohujumu miundombinu ya Serikali kuwa pindi watakapokamatwa, watachukuliwa hatua kali za kisheria kwa kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi.

Ameyasema hayo leo Septemba 19, 2025 alipokua akikagua maeneo ya katikati ya Jiji la Dodoma ambayo yameathirika na wizi wa mifuniko ya chemba za majitaka hali inayohatarisha usalama kwa watumiaji wa barabara pamoja na vyombo vya moto katika maeneo hayo kutoka na mashimo hayo kubaki wazi.

“Sisi Mkoa tumesikitishwa na jambo hili na tunaahidi watu hawa wataendelea kutafutwa kwa hatua zaidi na yeyote atakayeshikwa, atashtakiwa kwa kosa la Uhujumu Uchumi. Pia kuna baadhi ya maeneo tunasikia wanaiba nguzo za umeme za chuma, nitoe maelekezo kwa Wenyeviti wa Mitaa, Kata na Vitongoji waweke utaratibu maalum kwenye mitaa yao kuhakikisha mali hizi zinalindwa”. Mhe. Senyamule.

Mhe. Senyamule ameongeza kuwa, Mkoa utaunda timu ya Wataalam watakaofanya doria usiku na mchana kwenye mitaa mbalimbali ili kuwabaini na kuwakamata wezi wa miundombinu ya Serikali hivyo anatamani kila mwananchi awe mstari wa mbele kulinda mali hizo kwani Serikali imewekeza maendeleo makubwa kwa ajili yao.

Aidha, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Dodoma Mhandisi Aron Joseph ametaja changamoto hiyo kuigharimu Serikali kwani mpaka sasa mifuniko iliyoibiwa ni 61 ikiwa na thamani ya Shilingi Milioni 91 ambapo wanaoiiba huiuza kama vyuma chakavu.

Hata hivyo, Mhe. Senyamule ametoa wito kwa wananchi wanaotumia mashimo hayo kutupa takataka, kuacha mara moja kwani wanasababisha mashimo kujaa, kuziba njia ya maji taka na hatimaye kusambaa barabarani hali inayosababisha uchafuzi wa mazingira sambamba na magonjwa ya milipuko.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • DODOMA NI SEHEMU NZURI YA UWEKEZAJI

    October 01, 2025
  • CCTV CAMERA KUFICHUA WAVUNJIFU WA SHERIA KATIKA JIJI LA DODOMA

    September 30, 2025
  • DODOMA YAADHIMISHA SIKU YA UTALII DUNIANI KWENYE MICHORO YA MIAMBANI KONDOA

    September 27, 2025
  • JUHUDI KUDHIBITI VIFO VYA WAJAWAZITO ZAPAMBA MOTO

    September 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.