• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

BAHI WAHIMIZWA KUFANYA VIKAO VYA MAPATO NA MATUMIZI

Imetumwa : October 12th, 2022

Katika muendelezo wa ziara zake za kutembelea Halmashauri za Mkoa wa Dodoma, kwa lengo la kuongea na watumishi, kutembelea miradi pamoja na kufanya mikutano ya hadhara ili kusikiliza kero za wananchi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ametembelea Halmashauri ya Wilaya ya Bahi

Katika ziara hiyo Mkuu wa mkoa ameongozana na Katibu Tawala Mkoa Dkt. Fatuma Mganga, Kamati Kuu ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Wakuu wa Taasisi mbalimbali na Wataalam kutoka  idara  mbalimbali za Mkoa.

Mkuu wa Mkoa alianza ziara yake kwa kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi  ambao walipewa fursa ya kueleza kero zao, ambapo nyingi ya kero zao zilihusiana na TASAF, uwiano wa waalimu wa mjini na vijijini,upungufu wa madarasa, wanafunzi kutojiunga kidato cha kwanza, ukosefu wa huduma za maji,umeme na usafiri kwa baadhi ya maeneo.Mkuu wa Mkoa amesikiliza kero zao na kuzipatia majawabu kupitia kwa  wataalam na wakuu wa idara.

Akizungumzia Utawala bora, Mhe. Senyamule amesisitiza kwa mapana suala la uongozi bora na maadili kwa watumishi. “Rais wetu anaonyesha kwa vitendo dhima ya utawala bora lakini sisi huku ngazi za chini bado kuna shida. Nahimiza Viongozi mfanye vikao kila baada ya miezi mitatu, huko kwenye vijiji, watendaji fanyeni vikao vya mapato na matumizi kwani wananchi wengi hawapati taarifa”. 

“Kuna mambo matatu yanayoashiria utawala bora, ambayo ni mosi, kufanya vikao.Kitu kinachoonyesha kuwa hatuna utawala bora ni pamoja na kutokufanyika Kwa vikao. Wananchi hawajui miradi mbalimbali inayofanywa, wananchi wanatakiwa wajue miradi yao. La pili, ni kusikiliza kero za Wananchi , Serikali za vijiji mtendaji wa kijiji na kata sikilizeni kero za Wananchi.La tatu,Kuwa waadilifu. Uvunjaji wa maadili mfano kunywa pombe wakati wa saa kazi. Kila mtumishi anafahamu kuwa pombe inaruhusiwa baada ya saa za kazi  kuanzia saa 10 jioni katikati ya wiki na  wiki endi  kuanzia saa 8:00 mchana. Hivyo kiongpozi ukiwa mwadilifu ni rahisi kuwachukulia hatya wale wanaovunja sheria hivyo. Wale wote waoacha kazi na kunywa pombe muda wa kazi /mapema washikeni na kuwapiga faini”. Amesisitiza Mhe. Senyamule.

Aidha niwaagize Maafisa utumishi kuwapatia mafunzo watendaji kwani hii Itasaidia sana katika kuwakumbusha wajibu na majukumu yao. Mkuu wa Mkoa  amegusia, suala la usimamizi wa Miradi inayoanzishwa na Serikali kwani Rais amedhamiria kuwakomboa Watanzania hivyo miradi inapokuja isimamiwe kikamilifu na kuhakikisha inaisha kwa wakati.

“Naagiza, Maafisa Elimu Wilaya, Kata na Vijiji, simamieni ujenzi wa madarasa yaishe kwa wakati kwani Bahi ina madarasa machache kuliko Halmashauri zote sasa isiwe tena mnapitwa na wenye madarasa mengi wanamaliza kabla yenu” Mhe. Senyamule

Akizungumza kwenye kikao cha hadhara na wanachi wa Bahi Sokoni, baada ya kusikiliza kero za wananchi hao na kuzipatia majawabu kupitia kwa wakuu wa Idara alioongozana nao, Mhe. Senyamule amewataka wananchi wa Bahi kuchangamkia fursa mbalimbali zinazopatikana Dodoma

“Fursa zote zilizopo Dodoma ni za Bahi pia, kwani ipo miradi mbalimbali iliyoanzishwa na Serikali pale Dodoma mjini kama majengo ambayo yanahitaji wapangaji, kuna miradi inayohitaji watu wa kuwaajiri. Changamkieni fursa hizo” Amesisitiza.

Halikadhakila , Mkuu wa Mkoa ametoa maelekezo juu ya kero iliyowasilishwa na wananchi kuhusu Stendi  mpya iliyojengwa na Halmashauri kwani wanadai haina miundombinu na huduma za kujitosheleza za kijamii ambapo ametoa muda wa mwezi mmoja kuhakikisha miundo mbinu inakuwepo, vibanda kwa ajili ya wajasiriamali hapo stendi vijengwe, Idara ya maji ihakikishe imefikisha miundo mbinu ya maji pia TANROADS waweke alama ya kivuko cha watembea kwa miguu (Zebra Cross).

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.