• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Balozi wa zambia nchini tanzania mhe. Benson keith chali amtembelea mkuu wa mkoa wa dodoma mhe. Jordan rugimbana ofisini kwake, machi 17, 2017

Imetumwa : March 17th, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana Machi 17, 2017 amekutana na Balozi wa Zambia Nchini Tanzania Mhe. Benson Keith Chali  na kufanya nae mazungumzo mafupi juu ya utekelezaji wa azma ya Serikali kuhamia Makao Makuu ya Nchi Dodoma wakati Balozi huyo alipomtembelea Mkuu wa Mkoa ofisini kwake.

Katika mazungumzo yao, Balozi Chali amemhakikishia Mhe. Rugimbana kuwa Serikali ya Zambia inapongeza uamuzi huo wa Serikali ya Tanzania na Zambia itakuwa miongoni mwa Nchi kumi (10) za kwanza kujenga Balozi zake Mjini Dodoma na kuhamia. Ameongeza kuwa ujenzi huo utahusisha ofisi za ubalozi na makazi kwa ajili ya Balozi na wafanyakazi wa ubalozi akitambua kuwa Dodoma ni Mji unaokuwa kwa kasi na idadi ya watu inatarajiwa kuongezeka kwa kiasi kikubwa.

“Tanzania na Zambia zina mahusiano ya kindugu kwa miaka mingi tangu enzi za Mwalimu Nyerere na Rais wa zamani wa Zambia Keneth Kaunda” alielezea Balozi Chali na kuahidi kutoa ushirikiano unaowezekana pale utakapohitajika. 

 

Mhe. Rugimbana alimjulisha Balozi huyo kuwa Uongozi wa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikisha Wadau mbalimbali umepanga kujenga Miji mipya mitano (5) ya kisasa inayojitegemea kwa huduma na miundombinu yote muhimu (Satellite Cities). Aliongeza kuwa Miji hiyo itajengwa kwenye Wilaya zinazozunguka eneo la Manispaa ya Dodoma na mmoja utajengwa ndani ya Manispaa ya Dodoma.

Mhe. Rugimbana alimwelezea Balozi Chali kuwa mpango wa Mkoa katika ujenzi wa Miji hiyo utajumuisha majengo yanayoweza kutumika kama ofisi na makazi ambapo hata Balozi za Nchi mbalimbali zinaweza kupata maeneo ya kuendeshea shughuli zao Mjini Dodoma, na Nchi yoyote itakayotaka kujenga ubalozi wake Mjini Dodoma utaratibu utashirikisha Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.

Aliongeza kuwa katika Miji hiyo mipya kutajengwa nyumba za gharama nafuu kwa ajili ya kuwakopesha Wafanyakazi wa Serikali waliopo na watakaohamia Dodoma na kuwawekea utaratibu wa kulipia kidogo kidogo, lengo likiwa kuwawezesha Wafanyakazi wa Serikali  kuondokana na shida ya makazi na gharama za kupanga nyumba.

“Mpango uliopo pia utaboresha miundombinu ya muhimu kama barabara na kumalizia upanuzi na uboreshaji wa uwanja wa ndege unaotumika kwa sasa  mjini Dodoma na ujenzi wa uwanja mpya wa kisasa wa ndege  wa Msalato” alibainisha Mkuu wa Mkoa.


Kupitia kwa Balozi Chali, Mhe. Rugimbana aliwakaribisha Wawekezaji mbalimbali kutoka Zambia ambao wanataka kuwekeza Dodoma kwa kuwa Dodoma ipo katikakati ya Tanzania, kiuchumi inarahisisha uzalishaji na usambazaji wa bidhaa mbalimbali kwenye Mikoa ya kanda zote za Nchi ya Tanzania na hata Nchi jirani kama Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi, Kongo, Zambia, Malawi na nyinginezo.

Imetolewa na:

Jeremia Mwakyoma

Afisa Habari

OFISI YA MKUU WA MKOA DODOMA

Machi 17, 2017

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.