• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

BENKI YA USHIRIKA KUZINDULIWA RASMI MAKAO MAKUU YA NCHI, DODOMA APRILI 28,2025

Imetumwa : April 25th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Benki ya Ushirika Tanzania (COOP Bank of Tanzania) inatajwa kuwa ya kipekee kutokana na kusimikwa kwenye misingi ya Ushirika, uchumi shirikishi na maendeleo ya pamoja hivyo kuifanya kuwa chombo cha kuwezesha maendeleo ya kiuchumi kwa watu wa kawaida katika jamii.

Hayo yamebainishwa leo Aprili 25, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano Ofisini kwake Jijini humu juu ya uzinduzi rasmi wa Benki hiyo utakaofanyika Aprili 28, 2025 kwenye Kituo cha Mikutano Jakaya Kikwete huku Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Benki hii ni ya kipekee inayomilikiwa kwa ubia na Vyama vya Ushirika, wanachama wao, vikundi vya kijamii na Taasisi za Ushirika kutoka nchini. Ni Benki iliyosimikwa katika misingi ya ushirika, uchumi shirikishi na maendeleo ya pamoja. Kupitia mfumo wa umiliki wa hisa, kila Mtanzania anayo nafasi ya kuwa sehemu ya mafanikio ya benki hii ikiwa ni chombo cha kuwezesha maendeleo ya uchumi wa watu wa kawaida.”

Aidha, Mhe Senyamule ameongeza kuwa Benki hiyo inaanza rasmi kazi zake ikiwa na Matawi manne (4) katika Mikoa ya Dodoma, Kilimanjaro, Mtwara (Tandahimba) na Tabora, sambamba na mawakala zaidi ya 52 waliopo katika vijiji na miji mbalimbali nchini ambapo inaifanya kuwa karibu zaidi na wananchi hasa ambao hawajafikiwa na huduma za kifedha.

Kadhalika, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw. Godfrey Ng’urah, amesema Benki hiyo ni ya kibiashara kwa wanaushirika hivyo, itachagiza shughuli za kilimo, shughuli za kinamama, kuongeza thamani ya mazao pamoja na shughuli za biashara kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati pamoja na kurudisha enzi za ushirika katika nchi.

Uzinduzi huo utatanguliwa na Kongamano la Kitaifa la Wanaushirika Aprili 27, 2025 likiwa na mada kuu: “Tafakuri na Mijadala juu ya Historia, Changamoto na Fursa za Uwekezaji katika Sekta ya Ushirika kuchochea Ukuaji wa Uchumi na Kuondoa Umaskini” litakalozinduliwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.


#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

#karibumwengewauhuru2025mkoawadodoma

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.