• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

BENKI YA USHIRIKA TANZANIA KUCHAGIZA UKUAJI UCHUMI WA DODOMA

Imetumwa : March 26th, 2025

Na. Hellen M. Minja,      

       Habari – DODOMA RS      


Benki ya Ushirika Tanzania imefungua Ofisi zake za Makao Makuu Jijini Dodoma na kujipambanua kuwa itatengeneza mifumo itakayoendana na Dira za Mkoa na kuitofautisha na nyingine kwa kuchagiza kukuza uchumi wa wananchi wake.


Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw. Godfrey Ng’urah alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule Ofisini kwake katika Jengo la Mkapa Jijini Dodoma Machi 26, 2025.


Lengo la ujio huo ni kujitambulisha na kutambulisha Benki hiyo kuwa imehamia Mkoani hapa kwa kujenga Ofisi zake za Makao Makuu na wapo tayari kushirikiana na Mkoa katika kutekeleza vipaumbele vya Mkoa hasa kuinua uchumi wa wananchi wake kwa kuwawezesha wanawake na vijana.


Ameongeza kuwa Benki yake ni ya ushirika kwa maana ya kwamba wamiliki wakubwa wa hisa ni vyama vya Ushirika wanaomiliki zaidi ya asilimia 51 ya Benki, sekta binafsi mchanganyiko, watu binafsi (vyama), wajasiriamali na wafanyabiashara kwa 19%, Serikali kupitia TIRA wanamiliki 10%.


Mkuu wa Mkoa Mhe. Senyamule amesema; “Dodoma tuna kipaumbele mwaka huu ambacho ni kukuza uchumi wa wananchi kupitia kilimo ambapo 72% ya wanadodoma ni wakulima, utalii, kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa wa Kilojistiki (Logistic hub) lakini pia kupitia Madini ambayo aina nyingi zaidi yanapatikana hapa”


Benki hiyo ambayo inahusisha vyama vya ushirika vya kilimo na kifedha, imeshafungua matawi manne katika Mikoa ya Tabora, Mtwara (Tandahimba), Kilimanjaro (Moshi) na Makao Makuu yake Dodoma huku ikiwa kwenye mchakato wa kujenga matawi mengine katika Mikoa ya Dar es Salaam, Kagera na Mwanza.




#dodomafahariyawatanzania  

#wekezadodomastawishadodoma                          

#keroyakowajibuwangu  #mtiwangubirthdayyangu           

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.