• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

BILIONI 1.6 ZANUFAISHA WAKAZI WA CHAMWINO KATIKA SEKTA YA MAJI

Imetumwa : April 25th, 2023

Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amezindua mradi wa tenki la kuhifadhi maji safi lenye uwezo wa kuhifadhi lita za ujazo milioni 2.5 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambayo kilele chake ni tarehe 26/4/2023.

Mradi huo umegharimu jumla ya shilingi bilioni 1.6 badala ya 2.5 kutokana na usimamizi madhubuti na kuwezesha matumizi sahihi ya rasilimali fedha. Kukamilika kwa ujenzi wa tenki hilo kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji safi kutoka asilimia 42 mpaka 87 katika Wilaya ya Chamwino. Uzinduzi wa Mradi huo umefanyika leo tarehe 25/4/2023 katika eneo la Buigiri wilaya ya Chamwino jijini Dodoma

"Kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano ambayo yanafanyika kila mwaka tarehe 26, Aprili sisi tumeamua kama mkoa wa Dodoma kuzindua mradi huu mkubwa wa maji safi katika wilaya hii ya Chamwino ambayo ni wilaya ya kimkakati katika harakati za Serikali kuhamia Dodoma, tunawapongeza viongozi wetu kwa kuendeleza Muungano huu kwa namna nchi yetu ilivyopiga hatua na inaendelea kupiga hatua kwa kukuwa kwa miundombinu, kiuchumi na kuongezeka kwa watu

"Niwapongeza Ofisi ya Makamu wa Rais ambayo ndio inayohusika na usimamizi wa masuala ya Muungano kwa kuendelea kuondoa changamoto za Muungano na kuendelea kuboresha na kuufanya kuwa imara na kuvutia mataifa mengine ambayo yanaendelea kujiuliza siri ni nini ya Muungano huu kudumu kwa miaka mingi."Amefafanua Senyamule

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika ulinzi wa vyanzo vya maji, kutunza maji na kuhakikisha wanalipa bili za maji ili kufanya mradi kuwa endelevu.

"Niwapongeze watumishi na uongozi wote wa DUWASA mkiongozwa na Mhandisi Aron Joseph, kwa ubunifu huu wa kuokoa pesa nyingi za serikali kwa kubuni namna nzuri ya usimamizi wa ununuzi wa vifaa na kumkabidhi Mkandarasi ambaye ni SUMA JKT na yeye kutekeleza mradi huu kwa uaminifu mkubwa ukweli ni kwamba mmefanya kazi nzuri,"amesema Senyamule .

Aidha, Senyamule amewahakikishia wawekezaji wote wanaotaka kuwekeza Chamwino kuja kuwekeza kwani kuna uhakika wa upatikanaji wa maji endelevu hivyo ni eneo salama.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba amesema miradi inayotekelezwa ya uchimbaji wa Visima maeneo ya pembezoni ina thamani ya bilioni 4.8 katika eneo la Nzuguni ambao utazalisha maji lita milioni 7 kwa siku na unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti mwaka 2023. Amefafanua kuwa mradi mkubwa wa miji 28 Chamwino ikiwepo unaendelea na mkandarasi anaendelea kukamilisha kutakuwa na uhakika wa kupunguza changamoto ya maji.

Ili kuhakikisha matatizo ya maji yanapungua Jijini Dodoma serikali imeanza kufanya utafiti wa kutoa maji kutoka Bwawa la Mtera na Bwawa la Farkwa ambapo upande wa Bwawa la Farkwa tayari utaratibu wa kuwalipa wananchi fidia ya bilioni 7 unaendele na mradi huo ukikamilika utazalisha maji lita milioni 120 kwa siku.

Pia Wizara ya maji inaendelea kutimiza Malengo ya kimataifa ambayo ni kuhakikisha huduma ya maji inawafikia wananchi kwa asilimia 100 ifikapo mwaka 2030.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Bi. Gift Msuya amesema kwa niaba ya wananchi wake ameahidi kuendelea kusimamia miradi hii idumu na iweze kutoa huduma kwa jamii kama ilivyokusudiwa, pia kuendelea kuuenzi na kuulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.