• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

BILIONI 3.4 KULIPA FIDIA ZA ARDHI DODOMA

Imetumwa : January 9th, 2024

Serikali ya Mkoa wa Dodoma Chini ya Mhe. Senyamule imedhamiria wananchi wake kuishi kwa Amani na utulivu kwa kutatua kero na changamoto za wananchi ikiwemo kero zitokanazo na madai ya fidia za ardhi zilizotwaliwa kwa matumizi mbalimbali ya Serikali hivyo shilingi Bilioni 3.4 zimetolewa kwa dhumuni la kuwalipa fidia wananchi wa Jiji la Dodoma.

 Hayo yameelezwa Januari 8, 2024 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe . Rosemary Senyamule wakati  wa Uzinduzi wa mpango mkakati wa kushughulikia migogoro ya ardhi uliofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Mbabala katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

 Ni Katika hafla ya Uzinduzi wa ulipwaji fidia  ambapo umekabidhiwa mfano wa hundi yenye jumla ya shillingi 3,068,705,727.81 zitakazolipwa kwa wananchi 314 na malipo kufanyika baada ya uhakiki wa uhalali wa fidia na timu iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa, hatahivyo jumla ya wananchi 127 wanakidhi vigezo na wanalipwa jumla ya madai ya shillingi 1,735,901,727.81.

 Mhe. Senyamule ametumia jukwaa hilo kuwasihi wananchi kutunza mazingira kwa kuendelea kutekeleza ajenda  mbalimbali za mazingira ikiwa ni pamoja na kila kaya kupanda miti isyopungua mitano hususani katika msimu huu wa mvua.

 "Tuendelee kutekeleza kampeni mbalimbali za mazingira kwani zipo nyingi zikiwemo 'soma na mti' kila kaya kupanda miti si chini ya mitano na nyinginezo ili kukijanisha Jiji letu " ameeleza Mhe. Senyamule

 Pia, amesisitiza utunzaji wa Jiji la Dodoma kwa wananchi kuzingatia taratibu za mipango miji ikiwemo kufuata taratibu za ujenzi wa nyumba za makazi uliopangwa na Jiji ili kuhakikisha Unadhifu wa Jiji unazingatiwa.

 Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe.Jabir Shekimweri amewasihi wananchi ambao hawajajitokeza kuhakikiwa viwanja vyao,  wajitokeza ili waweze kulipwa madai yao sahihi na halali kwa mujibu wa makubaliano yao na Serikali.

 Mpango mkakati huo umetokana na kukithiri kwa migogoro ya ardhi ndani ya Jiji la Dodoma hali iliyopelekea Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuunda tume kwa ajili ya kuchunguza chanzo cha migogoro ya ardhi katika Jiji la Dodoma ambapo baada ya Tume hiyo kubaini changamoto mbalimbali ikiwemo kuchukuliwa kwa maeneo ya wananchi hao kwa matumizi na maslahi mapana ya Taifa ikabiriki Fedha hizo kulipwa kwa wote waliokidhi vigezo.

 Miongoni mwa kata zinazonufaika na fidia hizo ni pamoja na  Iyumbu, Chigongwe, Mbalawala, Makole, Zuzu, Kikombe, Mtumba, Chahwa, Miyuji na Msingi Mlimwa C ambazo zote zinapatikana ndani ya Wilaya ya Dodoma.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.