• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

CHAMWINO YAAGIZWA KUKAMILISHA KITUO CHA AFYA ITISO KWA WAKATI

Imetumwa : February 1st, 2023


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino Dkt. Semistastus Mashimba kuhakikisha mradi wa Kituo cha afya cha Itiso kinachojengwa Katika Kijiji cha Mapango, Kitongoji cha Makulu A unakamilika kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma za afya haraka kama ilivyo azma ya Serikali ya kujengwa kwa kituo hicho.

Mhe. Senyamule ametoa maagizo hayo wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho cha afya ambacho kinaonekana kusuasua licha mkataba wa kazi hiyo kubaki siku chache.

“Natoa maagizo kwako Mkurugenzi, hakikisha unasimamia kwa karibu ujenzi wa kituo hiki usiku na mchana maana mpaka leo ilitakiwa tukute baadhi ya majengo yaliyokamilika yakitoa huduma kwa wananchi wa eneo hili lakini kwa jinsi inavyoonekana hata kwa kipindi kifupi kilichobaki cha siku kumi na nne cha kumalizika kwa mkataba, bado Kituo hiki hakitaweza kutoa huduma kitu ambacho hakipendezi kabisa kwani Mhe. Rais  ametoa fedha kamili za ujenzi halafu mpaka sasa hakuna huduma iliyoanza kutolewa hapa” Senyamule alisisitiza.

Ujenzi wa kituo cha afya cha Itiso unaogharimu kiasi cha Shilingi Milioni 500 ambazo ni fedha za tozo za Serikali kuu, unatekelezwa kwa awamu mbili ambapo kwa sasa ujenzi upo kwenye awamu ya pili. Jamii ya kata ya Itiso imekua ikitumia zahanati ya Itiso kwa ajili ya huduma za afya kwa muda mrefu ila kutokana na uhitaji wa kukuza wigo wa utoaji huduma, Serikali iliamua kutoa fedha za ujenzi wa Kituo hicho kwenye kata hiyo yenye vijiji vinne ambavyo ni Solowo, Mapanga, Itiso na Ikombo.

Sambamba na kutembelea mradi huo, Mhe. Senyamule pia ametembelea ujenzi wa mradi wa Bwawa la umwagiliaji la Membe linalojengwa katika Kijiji cha Membe kata ya Membe, Tarafa ya Chilonwa katika Wilaya ya Chamwino. Mradi huo wa umwagiliaji unagharimu shilingi Bilioni 12 na litakapokamilika litachukua eneo lenye ukubwa wa ekari 388 na linatarajiwa kumwagilia mashamba yenye eneo la ukubwa wa ekari 8,000

Akiongea na wananchi wa Kijiji cha Membe kwenye eneo la mradi wa Bwawa, Mhe senyamule amesema;

“Miradi hii kwetu ni ya kimkakati kwani itasaidia wananchi kuondokana na njaa kwa kulima kilimo cha umwagiliaji wakati wote wa mwaka. Dhamira ya Mhe. Rais ni kuwajali wanachamwino, kwa kuwajengea Bwawa hili litakalowawezesha wanachamwino kufanya kilimo cha kisasa na kwa sababu anajua wanachamwino ni wakulima wazuri. Nitoe wito kwa wakandarasi wazawa, fanyeni kazi kwa uhakika maana Serikali imewaamini wakandarasi wazawa hivyo hakikisheni mnakamilisha kazi hii kwa uadilifu na weledi mkubwa” Amesisitiza Mhe. Senyamule.

Bwawa la Membe litakua na tuta lenye urefu wa mita 490.1 na sehemu yenye kina kirefu itakua na mita 19.8. Bwawa litakua na ukubwa wa mita za ujazo wa milioni 12 ambazo ni sawa lita Bilioni 12 za maji ambalo litawezesha shughuli za uzalishaji wa mazao ya kilimo kwa kufanyika mara tatu mpaka nne kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Hata hivyo, ziara ya Mkuu wa Mkoa haikuishia hapo bali ilifika pia kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino ambalo lipo kwenye hatua za mwisho za umaliziaji ambayo ni awamu ya sita. Ujenzi huo unatarajiwa kukamilika Septemba mwaka huu na kukamilika kwake kutawezesha watumishi wa Halmashauri kufanya kazi kwa ufanisi na kutoa huduma kwa jamii.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.