• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

CHEMBA YA MKOSHA SENYAMULE KWA KUPATA HATI SAFI

Imetumwa : July 14th, 2023


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kwa kupata hati safi katika kikao cha Baraza la Madiwani  kilichojadili taarifa ya mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa Fedha 2021/2022 .

Pongezi hizo amezitoa leo Julai 14, 2023 wakati wa kikao kazi cha Baraza la Madiwani katika Ukumbi wa Halmashauri hiyo Mkoani Dodoma.

"Halmashauri ya Wilaya ya Chemba ilikuwa na hoja 50 ambazo ambazo zimegawanyika katika sehemu tatu, hoja za mwaka jana 25, hoja za miaka iliyopita 25 na agizo la LAAC ambalo ni moja" ameeleza Mhe.Senyamule

Aidha, amesema kati ya hoja 50, 13 zimefungwa na 37 bado zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji chini ya Menejimenti ya Halmashauri chini ya usimamizi wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo.

Mhe. Senyamule amewaasa kufanya kazi kwa bidii,kuondoa tofauti baina yao na kutafuta namna nzuri ya usuluhishaji wa tofauti zao zilizopo ili kuleta tija katika kuwatumikia wananchi.

‘’Chemba ni miongoni mwa Halmashauri ambazo taarifa za septemba 2022 zinaonyesha kuwa na tofauti katika taarifa zenu hivyo jitahidini kutafuta namna inayofaa kupata usuluhishi ili ziweze kuendana ili kupunguza hoja za ukaguzi kila mwaka” Senyamule amesisitiza

Mhe.Senyamule amesisitiza kamati za fedha zinazokutana kila mwezi ziwe na agenda ya kudumu ya kujadili mwenendo wa ujibuji wa hoja za ukaguzi za Mkaguzi wa ndani ili Halimashauri kuondokana na changamoto ya kuwa na hoja nyingi zisizofanyiwa kazi .

Vile vile ameagiza Halmashauri hiyo kuweka mikakati ya kuhakikisha mapato yanaongezeka kufikia bilioni 2 kwa kufanya ubunifu mbalimbali wa vyanzo vya mapato.

Aidha amewataka kuhakikisha wanakamilisha Miradi ya maendeleo kwa wakati na ubora unaotakiwa ili kuendana na kasi ya viongozi wanayotoa hela ikiwa ni pamoja na miradi ya fedha za SEQUIP .

 

Kwa Upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Ally Gugu amewaasa Watumishi kuendeleza kushirikiana na Utawala vizuri ili kurahisisha utendaji na kufuata Sheria, taratibu, kanuni za utumishi wa umma bila kupoteza muda katika utendaji kazi .

Naye, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chemba Mhe. Sambala Said amesema kwa mwaka huu mpya wa fedha Halmashauri hiyo imejipanga kivingine kila sekta ili kuonyesha utofauti na miaka mingine kama ilivyo fahamika kadhalika ameahidi ushirikiano katika utekelezaji wa miradi ya serikali.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.