• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

"CHUO CHA UFUNDI DONBOSCO MFANO WA KUIGWA" RC SENYAMULE

Imetumwa : November 25th, 2022


Chuo cha Ufundi Don Bosco Mkoani Dodoma ni Chuo cha Ufundi Stadi,ambacho kipo chini ya Kanisa Katoliki. Hivi karibuni Chuo hicho kimefanya mahafali yake ya 36 ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akiwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.

Mahafali hayo yamejumuisha wahitimu 213 ambapo ni mchanganyiko wa wale waliokua wakisoma kozi ndefu na wengine kozi fupi katika fani ya umeme, kilimo, ufundi bomba, ufundi magari, uchomeleaji, mapishi, seremala, ushonaji n.k

Mhe. Senyamule amekipongeza chuo hicho kwa kuwa mfano wa kuigwa. “Don Bosco mmekua mfano kwa kushiriki katika michezo, uwezeshaji wa vifaa vya kufanyia kazi kwa wanafunzi wanaohitimu pamoja na kushirikiana na Serikali hususani Ofisi ya Waziri Mkuu Watu wenye ulemavu. Hongereni sana. Watu wenye ujuzi ndio wenye uwezo wa kufanya mabadiliko katika jamii. Serikali ina uelekeo wa kuwa na viwanda vingi ambayo vinahitaji wataalamu wenye ujuzi hivyo hata Halmashauri zetu zimeelekezwa kuwawezesha wanafunzi wanaomaliza vyuo vya ufundi” RC Senyamule

Pia ameongeza kuwa Serikali imeendelea kutengeneza fursa mbalimbali kwa vijana kama vile kuziamuru halmashauri kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa makundi yenye uhitaji kwenye jamii wakiwemo wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, hivyo amewataka wahitimu hao kujiunga kwenye vikundi ili nao waweze kuwa wanufaika wa mikopo hiyo itakayowawezesha kujiajiri kwa ujuzi walioupata chuoni hapo.

Bi. Prisca Byala, Afisa Elimu Msingi ambaye amemuwakilisha Afisa Elimu Mkoa katika Mahafali hayo, amesema mafunzo haya ni hazina kwa vijana na Taifa kwa ujumla na anaamini kuwa yatawanufaisha huko wanapokwenda hivyo hakusita kuishukuru Serikali kwa kuyapa kipaumbele mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana.

Kadhalika akiongea kwa niaba ya uongozi wa Chuo, Mkuu wa chuo hicho Mkoa wa Dodoma Father Boniface Mchami, amesema “Chuo kinawalea vijana katika maadili mema na ucha Mungu, chuo kina ushirikiano na vyuo vingine kupitia michezo, semina na shughuli mbalimbali. Tumefadhili vijana 67 wanaosoma hapa ambao hawana uwezo wa kulipa ada pia Chuo kimepata nafasi ya kushirikiana na kampuni 5 kutoka nchini Marekani zinazojishughulisha na uchimbaji wa mafuta na wametoa scholarship kwa wanafunzi wetu 10 pamoja na walimu wanne kwenda kwenye mafunzo ya mwaka mmoja nchini Marekani”. Amesema Father Mchami

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.