• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DKT MPANGO AZINDUA MCHAKATO WA MAANDALIZI YA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050

Imetumwa : April 3rd, 2023

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ametoa rai kwa Wizara zote, Taasisi za Umma, Idara Zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sekta Binafsi, Watanzania wanaoishi na Wadau wote wa maendeleo kutoa ushirikiano wa kutoa maoni na taarifa kwa timu ya Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ili uchambuzi uwe halisia na toshelevu.

Dkt. Mpango amesema hayo wakati wa uzinduzi wa Mchakato wa Maandalizi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete mkoani Dodoma leo tarehe 03 Aprili 2023. Amesema dira hiyo inatarajiwa kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi na kijamii ili kufikia lengo la kuwa Taifa lenye ustawi.

"Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha katika maandalizi ya Dira hiyo, Watanzania kutoka pande zote za nchi, kutoka matabaka mbalimbali ya maisha, makundi mahsusi kama Bunge na Mahakama yatapata nafasi ya kuchangia mawazo yao.

"Fursa ambazo hazijatumika ipasavyo hadi sasa na pamoja na kuzikamata fursa zinazochipukia, kuzingatia masuala ya elimu hususan sayansi, ufundi na ufundi stadi, utafiti na maendeleo, na ubunifu ili kukuza ujuzi na uwezo wa nguvukazi ya Taifa, namna ya kuvutia na kuasili teknolojia ili kukuza tija katika sekta zote za uzalishaji na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ikiwa pamoja na kuingia ubia wa kimkakati kuiwezesha Tanzania kuwapita washindani wake katika kipindi kifupi, "Amesema Dkt mpango

Dkt.Mpango ametaja hatua zilizopigwa na Tanzania hadi hivi sasa ikiwemo kujenga na kuimarisha utawala wa sheria, haki na demokrasia, Mhimili wa Mahakama kuimarisha kazi ya kutoa haki kwa wananchi pamoja na Serikali kuendelea kuzingatia sheria, mila na desturi za watanzania katika uendeshaji wa shughuli za kiserikali. Ameongeza kwamba uhuru wa vyama vya siasa na vyombo vya habari umeimarika pamoja na kupatikana mafanikio ya kuridhisha katika elimu ikiwemo kuongezeka kwa udahili wa wanafunzi katika ngazi zote kuanzia shule za msingi hadi vyuo vya elimu ya juu.

Kwa Upande wake Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kupitia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 imeweza kufanikisha hatua mbalimbali za kimaendeleo kama vile uboreshaji wa miundombinu , ongezeko la shule, ukuaji wa sekta ya michezo pamoja na ukuaji wa uchumi kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Awali akitoa taarifa ya Mchakato wa Maandalizi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Natu Mwamba amesema chimbuko la Maandalizi ya Dira 2050 imetokana na kuendeleza mafanikio yaliofikiwa kutokana na utekelezaji wa Dira 2025 pamoja na uhitaji wa mkakati utakaowezesha nchi kunufaika na maendeleo ya kiuchumi na kiteknolojia yanayoendelea kuibuka duniani.

Ameongeza kwamba Dira 2050 itahakikisha kuwa Tanzania inaendelea na mkakati utakaoainisha ajenda ya maendeleo ya nchi na mikakati mingine ya kikanda na kimataifa.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutekeleza Mpango wa miaka 25 ya Maendeleo na kukiri Dodoma inajivunia mafanikio hayo.

"Nimpongeze Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan na viongozi wote watangulizi wake kwa kuendelea kutekeleza mpango wa miaka 25 na sisi Dodoma tunajivunia Sana maendeleo makubwa yaliyotokea katika miaka hii yote, tutaendelea kuiweka historia kuwa ndani ya miaka hii 25 Makao Makuu ya Serikali yamehamia katika Mkoa wetu, " Amesema Mhe. Senyamule

Uzinduzi wa Mchakato wa Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Viongozi wa vyama vya Siasa, Wabunge, Wadau wa Maendeleo, Sekta binafsi , Mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali hapa nchini, Viongozi wa dini pamoja na wananchi.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.