• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DKT MPANGO AZIONYA HALMASHAURI UTOAJI WA MIKATABA KWA MAKAMPUNI YA USAFI YASIYO NA SIFA

Imetumwa : June 5th, 2023

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amelitaka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa kote nchini kuongeza nguvu katika kusimamia utekelezaji wa katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki hapa nchini

Makamu wa Rais ametoa maagizo hayo mara baada ya kuongoza zoezi la kufanya usafi katika soko kuu la wamachinga mjini Dodoma ikiwa ni katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani leo tarehe 5 Juni 2023. Amesema ni lazima kuhakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa kwa wanaokiuka maagizo hayo pamoja na kuwataka watendaji wote wanaohusika kusimamia kwa karibu uzalishaji na matumizi ya mifuko mbadala.

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa ni vema kuhakikisha mifuko yote inayozalishwa inaonesha taarifa za mzalishaji na kama inakidhi viwango vya ubora vilivyowekwa na mamlaka husika. Pia amesisitiza makampuni na watu binafsi wanaozalisha bidhaa za plastiki kuhakikisha taka zinazotokana na bidhaa zinazozalishwa zinakusanywa na kuondolewa.

Halikadhalika Makamu wa Rais amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha kampuni zinazopewa kazi za ukusanyaji taka ziwe na uwezo kufanya kazi hizo kwa ufanisi. Amekemea utoaji wa tenda za uzoaji taka kwa kampuni zisizokuwa na uwezo na zile zisizo na vitendea kazi vya kisasa na kuzitaka Halmashauri kuweka miundombinu ya uhakika ya ukusanyaji na usombaji wa taka katika mitaa na maeneo ya mikusanyiko kama sokoni, stendi na hospitalini.

Aidha Dkt. Mpango ametoa wito kwa wananchi kutambua wajibu walionao katika kutunza vyanzo vya maji, kuacha mazoea ya kutupa taka hovyo na kuagiza kila kaya kuwa na sehemu mahsusi ya kuhifadhia ama kuchomea taka. Amesema masuala ya kufanya usafi na utunzaji mazingira hayana mbadala kwa kuwa mazingira ndio uhai na yana mahusiano ya moja kwa moja na ustawi wa Taifa kiuchumi na kijamii.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo amesema suala la utunzaji na uhifadhi wa mazingira limeendelea kupewa kipaumbele hapa nchini ambapo kwa kutumia Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kaulimbiu yam waka huu imebeba ajenda ya utunzaji wa mazingira na kutunza vyanzo vya maji.

Dkt Jafo amewapongeza wanafunzi kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu kwa kujitoa kuhifadhi mazingira ikiwemo kampeni ya soma na mti yenye lengo la kuhamasisha upandaji wa miti mashuleni. Halikadhalika amewashukuru wadau mbalimbali katika jitihada zao za kuhakikisha suala la mazingira linapewa kipaumbele kwa maendeleo endelevu.

Zoezi la kufanya usafi katika soko kuu la wamachinga mjini Dodoma limewashirikisha viongozi mbalimbali, wananchi na watumiaji wa soko hilo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani kwa mwaka 2023 inasema “Pinga uchafuzi wa mazingira unaotokana na taka za plastiki”

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.