• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DODOMA KUHAKIKISHA WANAFUNZI WOTE WANAKUNYWA MAZIWA SHULENI

Imetumwa : September 28th, 2022

kudhimisha wiki ya unywaji maziwa Duniani. Taifa la Tanzania limeadhimisha huku msisitizo ukiwa unywaji wa maziwa  kwa  wanafunzi shuleni. Kitaifa maadhimisho hayo yamefanyika Jijini Dodoma  katika Viwanja vya Nyerere Square  kuanzia 26.9.2022 hadi 28.9.2022.

Mkuu wa mkoa Mhe.Rosemary Senyamule  ndiye ambaye ndiye amekua mgeni rasmi wa shughuli hiyo. Akizungumza  Mkuu wa Mkoa  amesema  Mkoa wa Dodoma upo tayari kutekeleza mpango huo kwa kuhakikisha kila mwanafunzi anapata glasi ya maziwa shuleni.

“Dodoma tupo tayari kuwa kama mfano kwa mikoa mingine katika utekelezaji wa zoezi hili na kuhakikisha kila mwanafunzi anapata angalau glasi moja ya maziwa akiwa shuleni kila siku”. Amesema  Mhe. Senyamule.

Zaidi ya nchi 70 ikiwemo Tanzania zinaadhimisha wiki ya Unywaji maziwa Duniani ambapo mpango wa kuhakikisha kila mwanafunzi anapata maziwa shuleni ulianza kutekelezwa nchini mwaka 2017 na mpaka sasa takribani shule 48 zimenufaika huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa “Faulu Mtihani kwa glasi moja ya maziwa kwa siku”

“Juhudi ziendelee ili kila mtoto afikiwe na mpango huu, kwani maziwa yana faida nyingi mwilini kwa Watoto hasa kiakili” Ameongeza.

Hata hivyo, mgeni rasmi ameendelea kusema kuwa Serikali inaendelea na juhudi za kuhakikisha sekta za kilimo, uvuvi na ufugaji zinafanya shughuli zake kisasa zaidi kwani mpaka sasa mikopo yenye thamani ya shilingi Milioni 275 imetolewa kwa wafugaji kwa lengo la kuimarisha ufugaji nchini.

Pia Serikali imesamehe kodi ya ongezeko la thamani kwa vifungashio vya maziwa hivyo Serikali inatarajia kuona gharama za maziwa na bidhaa zinazotokana na maziwa zinashuka bei ili kila mmoja aweze kutumia bidhaa hiyo kwa urahisi kwani mtu mmoja anahitaji kunywa angalau lita 200 za maziwa kwa mwaka lakini kwa takwimu zilizopo sasa, mtu mmoja anakunywa lita 60 tu.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya mifugo na uvuvi Dr. Charles Mhina amesema lengo la siku hii ni kuhamasisha unywaji wa maziwa hasa kwa Watoto waliopo shuleni. Ameongeza kwa sasa lita za maziwa zipatazo Bilioni 3.4 zinazalishwa nchini lakini bado watanzania hatunywi maziwa.

“Tunapanga utaratibu wa kuwawezesha wadau kupatikana kwa kiasi kikubwa cha maziwa kukidhi idadi ya wanafunzi wote waliopo shuleni” Dr. Mhina

Siku ya unywaji maziwa shuleni inatekelezwa kufuatia wito wa Shirika la Chakula na kilimo ulimwenguni (FAO) ambapo kwa Tanzania, Bodi ya maziwa nchini (TADB) ambayo inaratibu mpango huu ikiwemo kufanya kampeni mbalimbali za uhamasishaji unywaji maziwa shuleni ambapo wadau mbalimbali wamejitokeza na wanaendelea kujitokeza kufadhili mpango huu kwa kugawa maziwa kwa wanafunzi kila siku ambapo mpaka sasa paketi 299 zimeshagawiwa kwenye shule kadhaa huku lita 6500 zikipokelewa kutoka kwa wadau hao.MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.