• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DODOMA NA MIKAKATI MADHUBUTI YA KUKUZA UCHUMI

Imetumwa : December 19th, 2024

Na. Sizah Kangalawe 

Habari- Dodoma Rs

Uchumi wa  Wananchi wa Mkoa wa Dodoma unaendelea kukua siku hadi  siku kutokana na uwepo wa ujenzi  wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita Mkoani hapa, hali inayosababisha Jiji la Dodoma kukua kwa kasi.

Ni katika kikao kazi cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dodoma (RCC), ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, ameweka bayana ukuaji wa Mji huu unaotokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuhamia kwa Makao Makuu ya Serikali na Ujenzi wa miradi mikubwa kama Uwanja wa Ndege Msalato na treni ya mwendokasi (SGR).

Kikao kazi hicho kimefanyika Desemba 19, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Vizano hoteli Jijini Dodoma.

"Mimi nikitembea Dodoma kila siku nakuta miji mipya imeanzishwa na Wananchi, wengine wanahitaji barabara na maji, hii inaonesha kuwa Mji wa Dodoma unakua kwa kasi.Bado tunajivunia miradi ambayo imetumia Fedha nyingi sana za Serikali, lengo kuu la miradi hii ni kuimarisha uchumi wa Mkoa wa Dodoma, lakini pia uchumi wa Serikali yetu.

Sisi Mkoa tunatakiwa tufikiri tunakwenda kufanya nini ili tuone tunaongezaje kipato cha mtu mmojammoja kupitia miradi hii mikubwa ambayo Mhe.Rais wetu amewekeza fedha nyingi katika miundombinu, sisi tunaongezaje kipato cha Taifa kupitia miundombinu hii ? yaani tunaweza kupata faida gani kupitia miradi hii", amebainisha Mhe. Senyamule

Aidha Mhe. Senyamule amezitaka Halmashauri zote za Dodoma zitafute njia mbalimbali za kukuza uchumi, huku akiwasihi Wanadodoma  mmoja mmoja kujishughulisha katika kazi mbalimbali zitakazowasaidia kujipatia kipato na kukuza uchumi wao,kadhalika uchumi wa Mkoa.

Naye Kanali Mstaafu Joseph     Simbakalia amevitaja vitengeneza fursa ambavyo vinapaswa kutumika ipasavyo ili kukuza uchumi kuwa ni Malikale, Mkao wa kijiografia, jua na upepo, hali ya hewa, madini, maji, ardhi, Makao Makuu ya Serikali, uongozi bora, miundombinu wezeshi na uwepo wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Utafiti, miundombinu saidizi ( masoko, minada na majengo ya biashara nk).

Katika hatua nyingine, Mhe. Senyamule ametumia kikao hicho kumkabidhi barua ya kumtambulisha Bw.Japhet P. Konzo, Mtanzania anayeishi Nchini China kuwa Balozi wa Dodoma Nchini humo ambaye atautangaza Mkoa na fursa zote zinazopatikana.

Akizungumza baada ya utambulisho huo amesema" nichukue nafasi hii kumshukuru Mkuu wa Mkoa na Serikali ya Mkoa wa Dodoma kwa kunipa nafasi ya kuwa Balozi wa Mkoa Nchini China, nchi ambayo imeendelea sana kwenye masuala ya teknolojia.

Mimi kama Balozi nitajitahidi kuona ni kwa jinsi gani naweza kuleta teknolojia hizo katika Mkoa wetu ili tuhakikishe kwamba tunaongeza tija kwenye masuala ya kilimo kwa kutumia teknolojia", amesema Bw. Konzo

Kikao kazi hicho kimefanyika Mwenyekiti akiwa ni Mkuu wa Mkoa, na wajumbe  ni Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakuu wa taasisi zilizopo ndani ya Mkoa, Wabunge na Wadau mbalimbali wa Maendeleo.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.