• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DODOMA YAHITIMISHA JUMA LA WADAU WA ELIMU

Imetumwa : March 25th, 2024

Mkoa wa Dodoma umefanya Mkutano wa wadau wa Elimu Mkoa Leo Machi 25, 2024 ikiwa ni kilele cha Juma la wadau wa Elimu lililozinduliwa rasmi Machi 19. Mkutano huo umehudhuriwa na mgeni rasmi, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa TAG Mipango, Jijini Dodoma.

Lengo hasa la Mkutano huo ni kujadili namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Elimu Mkoa wa Dodoma pamoja na kuweka mikakati ya kuinua Taaluma na ufaulu kimkoa pamoja na kuzindua rasmi Mpango Mkakati wa Elimu Mkoa wa DodomWaziri Mkuu ameipongeza Dodoma kwa kuandaa Mkutano huo kwani unakwenda sambamba na Sera ya Elimu ya nchi.

"Kauli mbiu ya Mkutano huu inakwenda sambamba na Sera ya Elimu ya nchi inayosisitiza Uwajibikaji. Utoaji wa Elimu Bora ni vipaumbele vya nchi. Serikali yetu inaimarisha mazingira ya utoaji Elimu kwa kuboresha miundombinu na Elimu bila ada kwani mpaka Sasa shilingi Trilioni 1 zimetolewa kufanikisha hili.

"Niwasihi Maafisa Elimu Kata kufuatilia maendeleo ya shule zenu kila wakati kwa kuwatembelea walimu wenu na kusikiliza kero zao. Walimu nanyi hakikisheni munafanya tathmini ya uelewa wa wanafunzi kwa kuwapatia mazoezi mengi kadri inavyobidi. Fedha zinazotolewa kwa ajili ya maendeleo ya Elimu, zitumike kwa ajili hiyo". Amesisitiza Mhe. Majaliwa.

Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amesema Serikali ya awamu ya Sita imefanya mambo mengi kwenye sekta ya Elimu.

"Tunamshukuru Rais kwa kuinua sekta ya Elimu Dodoma kwani tumeimarika sana miaka hii 3. Dodoma imepanda ufaulu wa darasa la 7 na kuingia kumi Bora kitaifa 2022 kwa ufaulu kupanda kutoka 83% (2022) hadi 87%(2023). Tumeanza kuweka mikakati ya Mkoa kuhakikisha kila mwaka ufaulu unapanda.

Pia ametaja mafanikio yaliyopatikana kipindi hiki kuwa ni ujenzi wa miundombinu ya Elimu iliyogharimu shilingi Bilioni 92.4 , miradi ya BOOST shilingi Bilioni 10.6 iliyowezesha ujenzi wa Madarasa 196 na matundu ya vyoo 154. Fedha nyingine ni kutoka miradi ya SEQUIP, SWASH, TEA , EP4R na mingine mingi ambayo kwa pamoja imeboresha kiwango cha Elimu.

Mkutano wa wadau wa Elimu Mkoa wa Dodoma umefuatia matukio kadhaa yaliyofanyika kwa Juma zima ikiwemo kukimbia mchaka mchaka kwa wanafunzi, uzinduzi wa Bonanza la michezo, ugawaji wa mipira 1000 kwa shule za Msingi za Mkoa kutoka Shirikisho la michezo nchini (TFF).

Pia Juma hili limewezesha uzinduzi wa kwaya ya Mkoa wa Dodoma, midahalo kwa wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari na kufunga mafunzo kwa wahitimu wa skauti Mkoa.

Juma la wadau wa Elimu Mkoa wa Dodoma limefikia kilele chake likiongozwa na kauli mbiu ya "Uwajibikaji wangu ni msingi wa kuinua ubora wa Elimu na ufaulu Dodoma".



#Keroyakowajibuwangu

#Dodomafahariyawatanzania













ReplyForward


Add reaction










Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.