• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DODOMA YAJIPANGA KIVINGINE KUBORESHA ELIMU

Imetumwa : January 5th, 2023

DODOMA YAJIPANGA KIVINGINE KUBORESHA ELIMU

Idara ya elimu Mkoa wa Dodoma imefanya kikao kazi cha wadau wa elimu Mkoa kilichohudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akiwa ndiye mgeni rasmi wa kikao hicho kililichofanyika katika ukumbi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) eneo la Mipango Jijini Dodoma.

Katika kikao hicho kilicholenga kujadili mpango kazi wa muelekeo wa namna ya kuanza mwaka mpya wa masomo 2023, kimejadili mambo mbalimbali yanayohusu mustakabali wa Elimu kwa Mkoa wa Dodoma na kupanga mikakati ya kufanya vizuri kwa mwaka huu mpya.

Mkuu wa Mkoa amebainisha mambo kadhaa ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameboresha kwa kiasi kikubwa kwenye sekta ya elimu.

“Rais amefanya mambo mengi kuboresha sekta ya elimu kama vile kuondoa ada kuanzia shule za awali mpaka kidato cha sita, ujenzi wa madarasa ya kutosha kupokea idadi kubwa ya wanafunzi wa kidato cha kwanza ambapo kwa awamu ya kwanza ya fedha za Uviko – 19 mwaka 2021 Mkoa wa Dodoma ulipata fedha za kujenga madarasa 776 na kwa mwaka huu tumepatiwa fedha shilingi Bilioni 15.6 kujenga madarasa 339. Pia Rais ametoa ruzuku kwa shule kila mwezi shilingi Milioni 200” Amesema Mhe. Senyamule

Aidha, Mkuu wa Mkoa ametoa hamasa kwa walimu kufanya kazi kwa bidii kwani wao ndio wanaoweza kusaidia kuinua Mkoa katika kupata matokeo mazuri kwenye mitihani ya kitaifa

“Nasisitiza walimu ni kundi linaloweza kujenga nchi au kuibomoa. Nitoe rai kwa maafisa na walimu wakuu kusimamia uandikishwaji wanafunzi wa shule za awali na darasa la kwanza. Mpaka sasa wanafunzi walioandikishwa kwa shule za awali wamefikia 57,617 ambapo lengo ni kuandikisha wanafunzi takribani elfu 70 na kwa darasa la kwanza wameandikishwa wanafunzi 74,230 sawa na 82.4% wakati lengo ni kuandikisha wanafunzi 90,122 hivyo uandikishaji haujafikia lengo. Niwatake Halmashauri zote kufuatilia uandikishwaji ili tuweze kufikia asilimia 100 kwani Watoto bado wapo wengi amabo hawajaandikishwa” Amesisitiza Mhe. Senyamule

Pia amezungumzia suala la utoro na kuwataka viongozi wote wanaohusika na ufuatiliaji wa wanafunzi kuhakikisha wanafunzi wote watoro wanarudi shuleni.

“Hakikisheni wanafunzi wote wanawasili shuleni na tuwahimize wazazi na walezi kuwanunulia wanafunzi mahitaji ya muhimu. Takwimu za utoro kwa mwezi Oktoba mwaka jana zilikua wanafunzi 18,883 hivyo, nawataka walimu wakuu kuwasilisha ripoti ya utoro kwa watendaji wa Kata kila Ijumaa ya wiki. Watoro wote warudi shuleni na wakaririshwe, jambo hili walimu mulichukulie kwa uzito kwani tumedhamiria kupambana na utoro mwaka huu” Amesema Mhe. Senyamule.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.