• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DODOMA YATENGENEZA MIKAKATI YA UWEKEZAJI

Imetumwa : October 18th, 2023


Wito umetolewa kwa wadau wa uwekezaji wa ndani Mkoa wa Dodoma kuchangamkia fursa za kihuduma zinazoendana na hadhi ya makao makuu kwani zipo nyingi.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule ambaye ndiye mgeni rasmi, wakati wa hotuba yake ya ufunguzi wa semina ya kujengeana uwezo wa uwekezaji iliyoandaliwa na Taasisi ya Uwekezaji Tanzania (TIC) Kanda ya kati kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Semina hiyo ya siku moja imefanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma iliyopo kwenye jengo la Mkapa ambapo wadau mbalimbali wameshiriki wakiwemo sekta za Elimu, vituo vya mafuta, Hoteli, usafirishaji, viwanda, Taasisi za fedha na nyingine nyingi ambapo wamepata nafasi ya kujifunza juu ya fursa na mabadiliko ya Sheria ya uwekezaji ya mwaka 2022.

Mhe Senyamule amesema kuwa wawekezaji wa ndani wana nafasi kubwa katika kukimbilia fursa hizi zinazojitokeza hasa kwa Mkoa wa Dodoma ambao upo kimkakati zaidi.

"Dodoma ni Mkoa ambao unakua kwa haraka kiuwekezaji kwani upo katikati ya nchi hali inayoufanya kuwa rahisi kufikika kwa watu kutoka mikoa yote ya Tanzania na pia ni makao makuu ya nchi. Fursa za uwekezaji kihuduma hapa Dodoma zipo nyingi zinazotakiwa kuendana na hadhi ya makao makuu. Tuanze kuifikiria Dodoma kama Mkoa wa kimkakati kwa kuwa na miundombinu toshelevu ambayo inaendelea kujengwa. Tunaendelea kutengeneza mkakati wa uwekezaji kwa Mkoa wa Dodoma hivyo tunawategemea sana nyinyi wawekezaji wa ndani" amesema Mhe. Senyamule

Aidha, Mhe Senyamule amesema semina hii ni sehemu ya utekelezaji wa kujengeana uwezo wa wawekezaji wa ndani pamoja na kukuza kada ya uwekezaji kwani matamanio ya Serikali ni kufikia Uchumi wa juu hivyo kundi la wawekezaji ni la kimkakati katika kufikia malengo hayo na ndio sababu kubwa ya Mhe. Rais kuanzisha Wizara ya uwekezaji ili kutafuta idadi kubwa ya wawekezaji watakaowekeza hapa nchini.

Meneja wa TIC Kanda ya kati Bw. Venance Mashiba amesema lengo kuu la kutoka semina hii ni kutoa Elimu juu ya uwekezaji, kufahamishana maboresho ya Sheria ya uwekezaji ya mwaka 2022 iliyokuja na mabadiliko kwenye sekta ya uwekezaji, kupashana habari miongoni mwa wawekezaji, kufahamiana kwa wadau wa uwekezaji waliowekeza ndani ya Mkoa wa Dodoma.

Semina hii inatarajiwa kuwa na tija kwa pande zote mbili yaani kwa Serikali na kwa wawekezaji wenyewe kwani mazingira ya kufanya kazi nchini ni mazuri ambayo huvutia wawekezaji wa nje kuingia kwa wingi na hii inatokana na utashi wa Serikali ya awamu ya Sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekua chachu ya kushawishi wawekezaji wa nje kuvutiwa na Tanzania ingawa dhamira yake ni wawekezaji wa ndani kukimbilia fursa hizi zaidi.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.