• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DSW WATAMBULISHA MRADI WA REST III KWA HALMASHAURI ZA BAHI NA DODOMA JIJI

Imetumwa : November 8th, 2024

Na. Hellen M. Minja,          

       Habari – DODOMA RS

Shirika lisilo la Kiserikali la Afya na Maendeleo kwa vijana (DSW)Tanzania, leo Novemba 8, 2024, limefanya kikao kazi cha mapitio ya Mradi wa REST unaojishughulisha na kujenga uwezo kwa Taasisi zisizo za kiserikali kuimarisha mifumo ya kijamii ili iwe na tija kwenye program zinazohusu afya ya vijana.

Kikao kazi hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Zabibu Jijini Dodoma, kimeshirikisha mashirika ya DOYODO, FAEF na WOWAP, viongozi wa Sekretarieri ya Mkoa wa Dodoma, viongozi na wataalamu kutoka Halmashauri za Bahi, Dodoma Jiji pamoja na wadau mbalimbali.

Mkurugenzi wa DSW Tanzania Bw. Peter Oaga, amezungumzia namna Shirika lake linavyoendelea na utekelezaji wa Mradi huo katika awamu yake ya tatu.

“Kwenye mpango wa REST, tunaendelea na utekelezaji, huu ni mwaka wa tatu na tunaendelea kwa miaka mitatu mingine. Tunaona kuna mabadiliko makubwa kwenye hizi taasisi, pia tumeona kuna matokeo chanya kwenye jamii kwani taasisi hizi zina ushirikiano mzuri na Serikali”Amesema  Bw. Oaga

Akizungumza kwa niaba ya Sekretariet ya Mkoa wa Dodoma, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa Bi Honorata Rwegasira, amesema Serikali ya Mkoa wa Dodoma ipo tayari kushirikiana na Shirika hilo katika utekelezaji wa mradi.

“Mlichokifanya na kukiongea hapa kiwe endelevu, sisi Serikali, tutaendelea kutoa ushirikiano katika maeneo yetu kwa kufanya ufuatiliaji kwani hiki kitu tunakifanya kwa mazuri na lengo ni kuisaidia jamii yetu, pale panapo hitajika ushauri wa kitaalamu msisite” Amesema Bi Rwegasira

Mradi wa REST unatekelezwa na DSW katika mikoa ya Arusha, Dodoma, Mwanza, Iringa na Mbeya kwa kushirikiana na Mashirika 11 ambapo kwa Dodoma unatekelezwa kwenye Halmashauri za Bahi na Dodoma Jiji kwa kushirikia na Mashirika ya DOYODO, FAEF na WOWAP.


#kurayakosautiyako              

#ujanjanikupigakura              

#dodomatukotayarikupigakura

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.