• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DUWASA YAPENDEKEZA ONGEZEKO GHARAMA ZA MAJI

Imetumwa : April 6th, 2023

Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) imetoa mapendekezo kwa Mamlaka ya udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) juu ya mabadiliko ya gharama za maji kwa watumiaji kwenye kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete na kufunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule

Katika kikao hicho, DUWASA imependekeza kupandisha gharama za utoaji wa huduma za maji kwa kufuata utaratibu wa TAFTISHI yaani Mkutano wa kukusanya maoni juu ya marekebisho ya bei ambapo wananchi ambao ndio watumiaji wa huduma hiyo wanapata fursa ya kutoa maoni yao juu ya bei pendekezwa.

Akizungumza katika kikao hicho Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Bw. George Kabelwa amesema DUWASA imeomba marekebisho ya bei za maji hadi mwaka 2026 ili kukidhi marekebisho ya miundombinu ya maji, kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi ili kukidhi matarajio ya Wana Dodoma. Ameongeza kuwa, licha ya sababu hizo za DUWASA, bodi ya EWURA baada ya kikao hiki ndio yenye wajibu wa kutoa jibu juu ya Maombi ya Mamlaka hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA Mhandisi Aron Joseph, akifafanua sababu za kuhitaji kurekebisha gharama za maji, amesema;

"EWURA imetaka kila Mamlaka kupitia bei zake kila baada ya miaka Mitatu na DUWASA haikua imefanya hivyo katika kipindi hicho. Hivyo kwa Sasa sababu kubwa zinazotufanya kufanya marekebisho ya gharama ni ili kuwezesha Mamlaka kumudu gharama za uendeshaji, katika kipindi cha miaka Mitano iliyopita, DUWASA haijafanya mapitio ya bei, kuongeza ufanisi wa DUWASA katika utoaji wa huduma bora, kuimarisha na kuboresha usalama wa maji yanayozalishwa na kusambazwa. Ongezeko hili limechangiwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya kiuchumi Duniani" Amesema Mhandisi Joseph.

Kadhalika Mhe. Senyamule amezungumzia uwekezajj Mkubwa wa Serikali katika sekta ya maji na kufafanua hali ya upatikanaji wa maji ilivyo sasa

"Serikali imekua ikifanya maboresho makubwa kwenye sekta ya maji ili kuongeza ubora na upatikanaji wa maji kwa asilimia 95 ifikapo mwaka 2015. Serikali inataka upatikanaji wa maji Vijijini ufikie asilimia 85 ifikapo mwaka 2025. Hali ya upatikanaji wa maji kwa sasa ni asilimia 50 Ila lengo ni kufikia asilimia 90.. Rais ameelekeza fedha nyingi kwenye miradi ya maji hivyo ni jukumu letu kuitunza miundombinu hiyo. Nitoe wito kwa wananchi, lazima tushiriki wote kwenye utunzaji wa maji ili tuweze kupata huduma bora" Amesema Mhe Senyamule

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.