• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

''HAKUNA MWANAFUNZI ATAKAYESHINDWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA KUKOSA MICHANGO''- RC-MTAKA

Imetumwa : June 17th, 2022


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Anthony Mtaka, amekutana na Walimu Wakuu wa shule za sekondari zenye kidato cha Nne na Sita ili kuongea nao namna ya kujiandaa na Elimu bure kwa kidato cha Tano na Sita.

Kikao hicho kilichohudhuriwa na takribani walimu wakuu 25 wa shule za sekondari za Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma ambazo zina  wanafunzi zaidi ya 3,000. Kikao hicho kiliainisha michango inayotozwa na shule ambayo huorodheshwa kwenye fomu ya kujiunga na Kidato cha Tano na ambayo kila mwanafunzi huhitajika  kuwa nayo pindi anapowasili shuleni kwa mara ya kwanza na kusababisha baadhi ya wazazi kushindwa kukidhi mahitaji hayo na kuacha kupeleka watoto shule.

Walimu hao walipata nafasi ya kuwasilisha changamoto zitakazowakabili baada ya ondoleo la ada hizo kwani zilikua zikisaidia katika uendeshaji wa shule hasa kulipia ankara za umeme, maji na wasaidizi wa majukumu ya shuleni na kuongeza kuwa mahitaji ya muhimu kama vile Bima ya afya, kuagiza vitendea kazi pamoja na vitabu vya kujisomea ndivyo hasa hupelekea wazazi na walezi kuona kwamba michango ni mingi inayotozwa na shule.

Mhe. Mtaka alisema kuwa Mhe. Rais Samia amefanya maamuzi ya kuondoa ada hizo ili wazazi waweze kupeleka watoto wao shule, bila kikwazo chochote."Elimu bila malipo itawaibua wale walioshindwa kufikika na wasiokua na mwanga wa elimu hivyo lazima tuwalinde Watoto wetu, utamaduni wetu na shule zetu"

Aidha Mkuu wa Mkoa alitoa maagizo kadhaa ikiwa ni pamoja na kila mwanafunzi aliyepangiwa kidato cha Tano  apokelewe kwa mazingira yoyote awe na michango au lah, michango yote inayotozwa na shule isizidi Shilingi 150,00/= kwa mahitaji ya muhimu, mwanafunzi asilazimishwe kununua vitu kwenye duka la shule, wanafunzi wasiwekewe masharti ya aina ya vifaa vya kupeleka shuleni.

Maagizo mengine ni pamoja na kuzitaka Idara za Elimu Mkoa, Halmashauri na Maafisa Elimu kukaa na kupanga mahitaji ya muhimu kwa shule zote na ziwe na kiasi kimoja. Kwa upande wa Bima ya afya, amesema atakaa na DMO kuangalia jinsi ya kuwasaidia wanafunzi watakaohitaji msaada na shule zisubiri mwongozo wa ada kutoka TAMISEMI ambao utatolewa hivi karibuni.

Wito umetolewa na Mhe. Mtaka kwa wazazi na walezi wote kupeleka watoto wote waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na ufafanuzi wa malipo ya ada wataukuta shuleni pia ametaka pasiwepo Mwanafunzi atakayeshindwa kuripoti shuleni kwa kukosa michango iliyopo kwenye fomu ya kujiunga na shule. Aidha Mhe. Mtaka  amewataka walimu kuendelea na moyo mwema wa kuwafundisha watoto kwani kazi yao ni kazi yenye haiba ya pekee na kazi ya Wito. Mwisho.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.