• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

HAKUNA SHERIA ILIYOWEKWA KUKANDAMIZA WENGINE RC SENYAMULE

Imetumwa : February 5th, 2024

Wito umetolewa wa Maafisa usafirishaji wa Bajaji na Pikipiki (Bodaboda) Jijini Dodoma kufuata sheria za barabarani zilizowekwa na Mamlaka husika ili kuepuka kadhia wanazozipata pindi wanapokua kazini. Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, alipokutana na kundi hilo kwenye ukumbi wa ofisi yake iliyopo jengo la Mkapa.

Mkuu wa Mkoa huyo, ameitisha kikao hicho ikiwa ni utaratibu wake wa kukutana na makundi mbalimbali ya kijamii yaliyopo ndani ya Mkoa wa Dodoma kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili. Katika kikao hicho, kero kadhaa ziliwasilishwa na nyingi zikapatiwa ufumbuzi ikiwemo ya uvunjaji wa sheria za barabarani ambapo amewataka madereva hao kufuata sheria kwa ustawi wa Mkoa.

“Sheria hizi zimewekwa ili tuzifuate na hakuna sheria iliyowekwa kwa ajili ya kumkandamiza mwananchi. Lengo hasa ni kuimarisha ulinzi na usalama wa raia. Nyinyi ni viongozi, kaeni na wenzenu munapokua kwenye vituo vyenu, peaneni ushauri wa namna ya kujiendeleza kwenye mambo ya msingi.

“Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anathamini makundi yote ya kijamii yaliyopo katika maeneo yetu na yote  anayapa uzito ulio sawa hivyo na sisi tunapaswa kufanya hivyo kwani Rais wetu anatamani kila mmoja awe na furaha.” Amesisitiza Mhe. Senyamule

Akijibu Baadhi ya kero zilizowasilishwa kwenye kikao hicho ambazo nyingi zililenga Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini LATRA inayojishughulisha na utoaji wa leseni za usafirishaji, Bw. Ezekiel Emmanuel ambaye ni Afisa Mfawidhi wa Mamlaka hiyo amesisitiza umuhimu wa kuwa na leseni ya usafirishaji ili kuepuka kadhia barabarani

“Mtu yeyote anayekusudia kufanya shughuli ya usafirishaji wa abiria, sharti nawe na leseni ya LATRA. Kinyume na hapo ni kosa la jinai na atapigwa faini ya shilingi 25,000. Tutii sheria bila shuruti kuepuka ukamataji holela. Tuhamasishane kwenye vituo vyetu kuepukana na haya. Tunatafuta riziki lakini sio kwa uvunjifu wa amani” Amesema Bw. Emmanuel.

Jiji la Dodoma lina takribani vituo vya Bajaji na Bodaboda 394 vilivyosajiliwa huku waendesha vyombo hivyo waliosajiliwa wakifikia takribani 400. Mkoa unathamini mchango wa sekta ya usafirishaji wa bajaji na bodaboda kwani unasaidia kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na Mkoa kwa ujumla

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.