• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

HALMASHAURI YA BAHI YAONESHA JUHUDI ZA KUINUA ELIMU KWA VITENDO

Imetumwa : April 18th, 2024


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule,  Aprili 18, 2024 ameshiriki hafla ya ugawaji wa vifaa vya shule kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mundemu wanaosomeshwa na Mfuko wa kusaidia na kuboresha Elimu katika Kata ya Mundemu Wilayani Bahi.

Hafla hiyo ya ugawaji wa magodoro na sare kwa wanafunzi hao, imefuatia Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Bahi kuanzisha mfuko wa kusaidia na kuboresha Elimu kwenye Halmashauri hiyo hasa kwa watoto wanaotoka kwenye familia zenye uhitaji.

Lengo hasa la mfuko huo ni kusaidia wanafunzi kuendelea na masomo kwa kuwafanikishia Mahitaji muhimu yanayohitajika kwa ajili ya Elimu kama vile ada, sare za shule, vifaa pamoja na fedha za kujikimu.

Mkuu wa Mkoa ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kuonesha juhudi za kuinua Elimu kwa vitendo.

"Bahi mumeonesha kujitambua, ukiiona Bahi umeona Elimu. Nyinyi mumetafuta utatuzi wa changamoto za Elimu kwani ndio kazi ya Serikali ya awamu ya Sita. Kusomesha watoto 1,036 kwa kuwalipia ada, sare za shule na fedha za kujikimu inawafanya watoto hawa waanze kufurahia masomo na kupenda kwenda shule". Amesema Mhe. Senyamule.

Mbali na hilo, Mhe. Senyamule ametoa maelekezo kwa Halmashauri nyingine za Mkoa wa Dodoma kuiga mfano wa Bahi kwa kuanzisha mifuko ya Elimu ili kusaidia wanafunzi wenye uhitaji kuweza kuendelea na masomo na kutimiza ndoto zao.

Pia ametoa wito wa kuhakikisha wazazi wa watoto wenye uhitaji na sifa za kuwa shuleni wanasaidiwa ili wafike shuleni.

Mfuko wa kusaidia na kuboresha Elimu Halmashauri ya Bahi, ulianzishwa Oktoba 2014 na unasaidia wanafunzi 1,036 umekua na mafanikio kadha wa kadha ikiwemo kumaliza tatizo la wazazi kushawishi watoto kujifelisha, kuongeza ufaulu, kuongeza idadi ya wasomi, kuongeza hamasa ya Elimu, kutoa magodoro 49 kwa wanafunzi wa bweni n.k.


























Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.