• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

HALMASHAURI YA JIJI DODOMA YAPOKEA MAPIPA 100 YA KUWEKEA TAKATAKA KUTOKA BENKI YA NMB

Imetumwa : June 16th, 2022

Halmashauri ya Jiji la Dodoma hivi  karbibuni imepokea mapipa 100 ya kuhifadhia takataka kutoka kwa Benki ya NMB. Mapipa hayo yatawekwa katika maeneo mbalimbali ya Jiji kwa lengo la kuimarisha usafi. Zoezi la ugawaji wa mapipa hayo  limefanyika katika viwanja vya Nyerere Square.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkuu wa Mkoa  wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka, amesema sasa umefika wakati muafaka wa  ajenda ya usafi kwa Jiji la Dodoma ibebwe kwa uzito kwa kila mmoja kuwajibika hasa kwa watendaji wa Mitaa ambao wanakabidhiwa mapipa haya kwani wanatakiwa kuhakikisha wanasimamia suala la usafi katika maeneo yao likienda sambamba na utunzaji wa mapipa haya ili yaweze kudumu kwa muda mrefu.

Amesisitiza kuwa, Sheria ya kuwawajibisha wale wote watakaobainika kuchafua Jiji izingatiwe na ndio maana Mahakama ya Jiji inaanzishwa na moja ya jukumu lake  itakua kusimamia suala la uvunjifu wa sheria ya usafi. Mhe. Mtaka  amemtaka msimamizi wa sheria za usafi za Jiji kuhuisha sheria zake ili zianze kutumika sasa aidha, ameitaka idara ya usafi wa mazingira iliyopo chini ya Halmashauri iweze kusimamia suala la usafi na matokeo yaonekane kwani anataka wananchi wa Dodoma wafikie mahali wawe na utamaduni wa usafi.

Naye Katibu Tawala Mkoa Dkt. Fatuma Mganga, alipata fursa ya kutoa neno wakati wa makabidhiano hayo ambapo aliishukuru benki ya NMB kwa kuona umuhimu wa kuweka jiji la Dodoma katika hali ya usafi na ameahidi kuhakikisha usimamizi na utunzaji wa mapipa hayo ili yaweze kudumu na kusema kuwa benki hiyo imeamua kushughulika na afya za wananchi wa Dodoma.

Akiongea kwa niaba ya Benki ya NMB ambao ndio wafadhili waliotoa mapipa hayo, Bw. Juma Kimori ambaye ni Afisa Mkuu wa Fedha, amesema kuwa Benki yake inapendezwa na jitihada za kuboresha Jiji la Dodoma kimazingira na imekua pamoja na mkoa katika kutekeleza kampeni ya kuifanya Dodoma ya kijani.

”NMB siku zote imekua na utaratibu wa kurudisha asilimia kadhaa kwa jamii na kwa mwaka huu imetenga kiasi cha  shilingi Bilioni 2.8 kwa ajili hiyo na imetumia shilingi Milioni 20 kwa ajili ya kununua mapipa ya takataka/Dustbins ambapo Mkoa unahitaji dustbins 350 lakini kwa sasa tunakabidhi 100 na juma lijalo tutakabidhi nyingine 50” Amesema Kimori.

Takribani Mapipa yakuhifadhia takataka 100 yamekabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma  ambaye naye ameyakabidhi kwa watendaji wa kata mbalimbali zinazopatikana katika Halmashauri ya Jiji Dodoma na kila Kata imepata mapipa 10. Mhe. Mtaka, amewaasa watendaji hao kusimamia utunzaji wa mapipa hayo na kubwa zaidi suala la usafi kwani hatosita kuwawajibisha endapo watakwenda kinyume na matakwa ya msaada huo. MWISHO.

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.