• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

HALMASHAURI ZASAINI MIKATABA NA BENKI UTOAJI MIKOPO YA 10%

Imetumwa : February 6th, 2025

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS

Halmashauri  chini ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI, leo Februari 07, 2025, zimetekeleza agizo la Rais wa Tanzania kwa kusaini Mikataba na benki washirika inayohusu utoaji wa mikopo inayotokana na 10%  ya mapato ya ndani ya Halmashauri hizo ambayo hutolewa kwa vikundi vya  Wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu.

Hafla hiyo ya utiaji saini, imefanyika baina ya benki tatu washirika ambazo ni NMB, CRDB na Uchumi Commercial Bank na Halmashauri 10 zilizowakilisha Halmashauri nyingine 175 za Mikoa yote ya Tanzania Bara katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma jengo la Mkapa Jijini humu.

Waziri mwenye dhamana Mhe. Mohamed Mchengerwa, amesema huo ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kuangalia namna bora ya utoaji wa mikopo hiyo ili fedha hizo ambazo zimelengwa kuyakomboa makundi maalumu ziweze kuleta tija.

“Katika kutekeleza maelekezo hayo, ilionekana kuwa mikopo hii itolewe katika mifumo ya kibenki na mifumo iliyoboreshwa na ilionekana Serikali ianze kutoa mikopo hiyo kwa kushirikiana na Mabenki lengo likiwa ni kuongeza ufanisi katika usimamizi na kuibua yale yanayowasibu Watanzania wa kawaida, wanyonge na wenye vipato vidogo.”

Aidha, ameongeza kuwa, zaidi ya shilingi 234,000,000,000 ambazo ndio kiwango cha juu kabisa, zinatarajiwa kutolewa kwa njia ya mikopo na zinakusudiwa kwenda kwa wananchi wa chini kabisa kwa lengo la kuinua uchumi wao, vikundi na Taifa kwa ujumla.

Nae, Katibu Mkuu TAMISEMI Bw. Adolf Ndunguru, amesema “matamanio ya Mhe. Rais ni kuona ufanisi umeboreshwa katika utoaji wa mikopo hii ambayo aliitolea maelekezo yake mwezi Machi, 2023, hivyo ni mwanzo wa mapinduzi makubwa katika kuhakikisha inaleta matokeo yenye tija kuliko huko nyuma”.

Akitoa salamu za Mkoa wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewakaribisha wageni Mkoani hapa na kuwasihi kuchangia uchumi wa Mkoa kwa kununua bidhaa za Dodoma pamoja na kutembelea miradi mikubwa ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa hapa Makao Makuu ya nchi.

Vilevile, benki washirika wameishukuru Serikali kwa kuwachagua kwenye mradi huo na watahakikisha wanufaika wanapata mikopo kwa wakati na wale wenye vigezo wanahudumiwa kwa wakati pia huku wakiahidi kufuatilia mikopo hiyo irudishwe kwa wakati ili na wengine waweze kunufaika.


#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.