• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

"Hela Za Lishe Zifanye Shughuli za Lishe " Dkt. Fatuma Mganga

Imetumwa : October 25th, 2022

Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Dkt. Fatuma Mganga ameyasema hayo wakati wa kikao cha kujadili utekelezaji wa Viashiria vya Mkataba wa Lishe robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2022/2023, taarifa ambayo hutolewa kila baada ya miezi mitatu. Taarifa hii ni ya kipindi cha Julai hadi Oktoba 2022.

Dkt. Mganga amesisitiza kuwa vikao vya lishe viwe vikao vinavyoleta tija, kwani suala la lishe ni suala mtambuka.Tunapaswa kutoa taarifa sahihi ambazo zinaonyesha uhalisia.

Akitoa taarifa ya robo mwaka Bi. Adela Mlingi ameeleza kuwa Mkoa wa Dodoma una jumla ya shule 947 (shule za msingi na sekondari ), kati ya shule hizo 947, shule 830  ndizo zinazotoa chakula shuleni hii ikiwa sawa na 87.6%.

Akikazia umuhimu wa Watoto/wanafunzi wote kupata uji au chakula wakiwa shuleni, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma amewaelekeza wakurugenzi wa halmashauri zote saba za mkoa kuongea na wazazi wa wanafunzi kwenye Halmashauri zao ili kuja na utaratibu wa kuhakikisha angalau wanafunzi hao wanapata uji wa saa 4.00 asubuhi.

Aidha Dkt. Mganga amewakumbusha wakurugenzi na wadau wa Lishe kuwa tunaelekea msimu wa kilimo hivyo ni vyema shule zote za msingi na sekondari zikaandaa maeneo ya kulima, kuaanda mbegu za mtama mweupe, kunde, maharage na mahindi na kisha wanafunzi wapewe maeneo ya kulima ambapo chakula kitakachopatikana kitakuwa kwa matumizi ya shule. Pia Katibu Tawala Mkoa amewataka wakurugenzi kuwahusisha wadau kama WFP ambao  wanaweza kuwapatia mbegu bora.

“Kila Mkurugenzi aje na mkakati wa jinsi watoto wanavyoweza kula shuleni, Msimu huu wa kilimo shule zetu zote tulime, na tutafanya ukaguzi kwa kila halmashauri ”.Ameagiza Dkt.Mganga.

Hali kadhalika wadau walipata fursa ya kuwasilisha taarifa za Taasisi zao za robo mwaka ambapo Bi. Edina Paul amewasilisha taarifa ya COUNSENUTH, kwa kueleza kuwa taasisi ya Counsenuth ilianza kazi 2018 na inafanya kazi katika vijiji 114 na kata 26 za Wilaya ya Chemba, ambapo shughuli zao kubwa ni kupambana na udumavu kwa vitendo. Taasisi hiyo imekuwa ikiendesha semima na warsha lakini pia wamekuwa wakiendesha elimu ya lishe kwa vitendo kwa kusisitiza wanafunzi walime mboga mboga mashuleni, kuhamasisha elimu ya afya kwa mama na mtoto.

Mdau, Doctors with Africa- Cuamm, taasisi inayojishunghulisha na lishe Wilaya ya Kongwa na Chamwino. Bi Flora Manyanda, ameeleza kuwa zaidi ya robo tatu ya gharama zao hutumika kwa ajili ya gharama za chakula na Dawa.

Baada ya uwasilishaji wa mada hizo mbili, mwenyekiti wa kikao hicho Katibu Tawala Mkoa amewataka wadau kuelekeza fedha zao kwenye  jambo /suala la lishe badala ya kutumia kiasi kikubwa cha fedha kwenye masuala ya posho.

“Tupunguze posho,na msisitizo uwe katika kutatua changamoto za lishe, watoto wanywe maziwa pia tuwe na mikakati ya kuhakikisha watoto wanakula shuleni, tuandae mbegu za kutosha za Mtama, Kunde, maharage, tukivuna tukaushe kwa matumizi ya baadae. Watoto wakipata uji au chakula shuleni itasaidia kupunguza utoro wa wanafunzi na kuongeza taaluma”. Amesisitiza Dkt. Mganga .

Aidha Dkt. Mganga amewataka wakurugenzi kuwakumbusha waalimu mashuleni uwepo wa ratiba ya vipindi vya dini.

“Walimu wanatakiwa kuhakikisha vipindi vya dini vinakuwepo kwenye ratiba na vinafundishwa kama vipindi vingine vya hesabu au Jiografia. Viongozi wa Dini Msisitie kuendelea kuwafundisha watoto wetu maadili ya mwenyezi Mungu. Kwa kufanya,

 hivyo mtakuwa mkitengeneza jamii bora ya kesho.”

MWISHO.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.