• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KAMATI YA BUNGE LAAC YATEMBELEA MIRADI WILAYA YA KONGWA

Imetumwa : March 14th, 2025

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS


Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Halima Mdee, imetembelea miradi miwili (2) inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Mkoa wa Dodoma Machi 14, 2025.


Akiikaribisha Kamati hiyo katika Mkoa wake ambayo pia ilianzia kwenye ofisi yake iliyopo Jengo la Mkapa Jijini humu, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amesema;


“Mkoa wa Dodoma umekua ukifanya vizuri katika miradi na vitu vingine hasa kupitia hoja za Mkaguzi wa Serikali, mara nyingi tumepata Hati safi japo haimaanishi hatuna kasoro, mambo mengi tumetakiwa kurekebisha ili tuwe safi zaidi ambayo ni kati ya haya mnayotaka kuyakagua kwani dhamira yetu ya kuhakikisha wanadodoma wanapata maendeleo ipo wazi”.


Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kongwa Dkt. Omari Nkullo, alitoa taarifa ya miradi miwili itakayotembelewa kwa kusema kuwa mradi wa kwanza ni ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri yake ambao unagaharimu kiasi cha shilingi Bilioni 3.5 na kwa sasa mradi umefikia 77% ya utekelezaji na unatarajiwa kukamilika 28/04/2025.


Katika Mradi wa pili ambao ni ujenzi wa miundombinu ya shule ya Sekondari Manungu iliyopo katika Kata ya Sejeli kupitia Mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari SEQUIP, mradi umekamilika na unafanya kazi ambapo jumla ya wanafunzi 304 wanasoma katika Shule hiyo,kati yao  Wavulana wakiwa ni 123 na Wasichana 181 kuanzia kidato cha 1 hadi 3.


Mradi umegharimu shilingi 544,225,626 ukijumuisha madarasa 8, jengo la Utawala, Maabara 3, Makataba 1, Chumba cha Kompyuta 1, matundu 10 ya vyoo, kichomea taka na tanki la ardhini kama ilivyoelekezwa na Serikali kuu. Mradi huu umesogeza huduma karibu na wananchi na kuwapunguzia mwendo wa Km 10 kila siku kufuata shule ya Sekondari eneo la Mbande.


Miradi yote imekaguliwa na Kamati hiyo na kupongezwa kwani inafanya vizuri huku wakimtaka Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa jengo la Halmashauri kuongeza idadi ya wafanyakazi ili uweze kukamilika kwa wakati uliokusudiwa na kutoa huduma kwa wananchi.


Baadhi ya maelekezo yaliyotolewa na Kamati kwa Afisa Masuhuri baada ya ukaguzi ni pamoja na usimamizi madhubiuti kwenye miradi na kuhakikisha inakamilika, kasi ya ujenzi wa jengo la Halmashauri iongezeke na kuhakikisha linakamilika ifikapo 30, June 2025, majengo ya TEHAMA  na Maktaba katika shule ya Sekondari Manungu ambayo yamekamilika yapatiwe vifaa na kuanza kutumika kufikia 30 June, 2025.


Akihitimisha ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya LAAC amesema; “Maelekezo ya Kamati ni sehemu ya Taarifa ambazo wakaguzi wenu watakuja kufuatilia utekelezaji wake hivyo, msipotekeleza haya, ofisi ya Katibu wetu itatoa taarifa hii ya maandishi kwa OR - TAMISEMI nao watawashushia. Ni muhimu kuyachukulia kwa uzito kwa sababu mukiyapuuza yatakuja kama sehemu ya maagizo ya Kamati yaliyopuuzwa na sisi tunakua wakali”. Mhe. Mdee.




#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.