• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KAMATI YA TATHMINI YA ATHARI ZA KODI NA TOZO YAFANYA UTAFITI DODOMA

Imetumwa : November 11th, 2024

Na. Hellen M. Minja,

       Habari – DODOMA RS

Kamati ya tathmini ya athari za kodi na tozo katika uendeshaji wa biashara nchini iliyoundwa na Wizara ya fedha ikiongozwa na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), leo Novemba 11, 2024 imefanya utafiti katika Mkoa wa Dodoma kwa kuzungumza na wafanyabiashara mbalimbali.

Utafiti huo uliofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Jengo la Mkapa Jijini Dodoma, umelenga kuainisha aina za kodi na tozo mbalimbali za Serikali ambazo ni sumbufu au hazina uhusiano na malipo ya mfanyabiashara.

Akizungumza wakati wa utafiti huo, Mchumi Mkuu kutoka TRA Bw. Aulelus Mnyamba, amesema utafiti huo umetokana na malalamiko ya wafanyabiashara juu ya utitiri wa kodi/ushuru/tozo katika Taasisi za Serikali.

“Waziri wa fedha aliona ni vyema kuiagiza Mamlaka ya Mapato ishirikiane na taasisi nyingine za Serikali kuainisha ni tozo zipi mnafikiri hazina msingi wowote au zina muingiliano, Taasisi mbili au tatu zinatoza kitu hicho hicho au ni kodi ipi ifanyiwe marekebisho” Bw. Mnyamba

Utafiri huo ulikwenda sambamba na majadiliano na michango tofauti tofauti kutoka kwa wadau na wafanya biashara ambapo wameshauri ili Serikali kupunguza utitiri huo wa kodi na kumpatia unafuu mfanyabiashara hasa mdogo aweze kukua, ni vyema kodi zote zikawekwa pamoja ambapo pia  zitarahisisha ulipaji wake.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir Shekimweri, amesema kuwa taasisi za ukusanyaji kodi zinatakiwa kuwa na maono ya namna ya kukusanya kodi bila kumuathiri mfanyabiashara.

Naye, katibu tawala msaidizi, seksheni ya biashara na uwekezaji Mkoa wa Dodoma, Bibi Mwajabu Nyamkomola amesema kuwa kutokana na kuundwa kwa Kamati hiyo, sasa kilio na changamoto za muda mrefu kwa wafanyabiashara, huo ndio muarobaini wake kwani maoni ya timu hiyo yatakwenda kufanyiwa kazi.


#kurayakosautiyako              

#ujanjanikupigakura              

#dodomatukotayarikupigakura

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.