• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KATIBU TAWALA SINGIDA AKABIDHI OFISI KWA KATIBU TAWALA DODOMA

Imetumwa : March 23rd, 2023

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga, amekabidhi Ofisi kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Senga Gugu aliyeteuliwa hivi karibuni na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo Dkt. Mganga amehamishwa kituo chake cha kazi.

Hafla ambayo imeshuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule kwenye ukumbi wa ofisi yake. Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo, Mhe. Senyamule amesisitiza juu ya majukumu ya msingi ya Katibu Tawala Mkoa pamoja na kugusia mambo mbalimbali ya kiutendaji yanayohusu ofisi yake;

"Katibu Tawala ndiye Msimamizi wa Usalama wa watumishi wote katika Mkoa hivyo tunatarajia usalama wetu utaendelea kuwa katika hali nzuri. Pia, Tumesitiza kwa Wakurugenzi wa Halmashauri kuwa kuvuka matumizi ya pesa za Serikali ni mwiko. Fedha za miradi zisivuke mwaka, ziende zikatumike kama ilivyokusudiwa. Nitoe shime kwa watumishi kuendelea kutoa huduma nzuri kwa wananchi. Nitoe mkazo pia katika kuimarisha usimamizi wa mazingira katika Mkoa wa Dodoma ili iendelee kung'aa kam ndoto za viongozi wetu zinavyotaka" Mhe. Senyamule

Akitoa neno la shukrani pamoja na kumuusia Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma juu ya kutoa huduma kwa wahitaji, Katibu Tawala Mkoa wa Singida amesema; "Namshukuru Mhe. Rais kwa kunipa tena nafasi nyingine ya kuwa Katibu Tawala kwani nimeonekana ninafaa kuendelea na nafasi yangu nikiwa Singida. Ofisi ya Katibu Tawala niliyoipata niliitumia kuwa faraja kwa watu kwani hapa ni Makao Makuu na watu wana shida nyingi, unapaswa kutumia mali yako kusaidia watu. Wakurugenzi Mimi nilikua Mtendaji na wakati mwingine niliwasukuma sana kwa lengo la Mkoa wetu uwe bora" Amesema Dkt. Mganga

Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu, naye akapata wasaa wa kusema machache wakati wa hafla hiyo; "Nashukuru sana kwa kunikabidhi kijiti hiki, nami nitatumia muda wangu kuhakikisha umoja huu ulioanza kuunganisha, unaendelea na kuimarisha mahusiano yetu na Taasisi mbalimbali. Tunayo fursa kubwa ya kuvutia wawekezaji na si kwenye kilimo na ufugaji tu, bali na sekta nyingine. Tushirikiane Mkoa wetu utoke kwenye nafasi za chini za uchangiaji wa pato la Taifa na kuwa kwenye nafasi juu" Amesema Bw. Gugu.

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.