• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KIKAO CHA UCHAGUZI WA WANAFUNZI WATAKAOJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2020 DODOMA, DISEMBA 06, 2019

Imetumwa : December 6th, 2019

RC DKT. MAHENGE AZIAGIZA HALMASHAURI MKOANI DODOMA KUHAKIKISHA ZINAKAMILISHA MAANDALIZI MUHIMU KWA AJILI YA KUWAPOKEA WANAFUNZI 33,803 WATAKAOJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MAPEMA MWAKA 2020

(Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma)

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote Mkoani Dodoma kuhakikisha wanakamilisha maandalizi yote muhimu kwa ajili ya kuwapokea wanafunzi wapatao 33,803 waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2020 kwenye shule za bweni na za kutwa Mkoani Dodoma.

Ametaja maandalizi muhimu ni pamoja na miundombinu ya elimu ikiwemo vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo na samani za shule. Amesema ufaulu katika Mkoa wa Dodoma kwenye mtihani wa kuhitimu elimu ya Msingi (Darasa la saba) kwa mwaka 2019 umepanda kufikia asilimia 74.69% ikilinganishwa na asilimia 70.45% ya mwaka 2018 ambapo kwa mwaka huu 2019 wanafunzi wote 33,803 waliofaulu darasa la saba wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza hali ambayo inachangia kuongezeka kwa mahitaji ya miundombinu hiyo ya elimu.


Dkt. Mahenge ametoa maagizo hayo Ijumaa Disemba 6, 2019 wakati akifungua kikao cha uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza mwaka 2020 katika Mkoa wa Dodoma ambapo ametumia muda huo kubainisha kuwa Halmashauri za Mkoa wa Dodoma zinakabiliwa na upungufu wa meza na viti 15,379, vyumba vya madarasa 153 huku akizitaja Halmashauri zenye upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa kuwa ni Halmashauri ya Wilaya Kongwa yenye upungufu wa vyumba 39, Mpwapwa vyumba 33, Chamwino vyumba 32 na Dodoma Jiji vyumba 22.

“Nawaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote kuhakikisha kuwa, kabla ya shule kufunguliwa Januari 6, 2020 miundombinu hii ikiwemo vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo na samani za shule yaani viti na meza iwe imekamilishwa kulingana na mahitaji ya kila shule” aliagiza Dkt. Mahenge.

Katika hatua nyingine Dkt. Mahenge amewataka Viongozi Wote wa Wilaya za Mkoa wa Dodoma, Viongozi wa Halmashauri zote Mkoani Dodoma na Viongozi wa Serikali za Mitaa kwenye Kata, Mitaa, Vijiji na vitongoji vyote kushirikiana na waratibu elimu kata, wakuu wa shule na wazazi Mkoani Dodoma kuhakikisha wanakomesha tatizo la utoro wa wanafunzi mashuleni na kuwataka wazazi na walezi watakaoruhusu watoto wao kuwa watoro wachukuliwe hatua.

“Nilifanya ziara kwenye Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma kukagua shughuli za elimu nikabaini moja ya tatizo kubwa lililopo mashuleni ni utoro wa wanafunzi” alibainisha Dkt. Mahenge huku akiwataka Viongozi na Watendaji wanaohusika kusimamia sekta ya elimu kwenye kila Wilaya kuhakikisha wanafunzi wote 33,803 waliofaulu darasa la saba na kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wote wanaripoti mashuleni ifikapo Januari 6, 2020 na pia kudhibiti utoro kwa wanafunzi wa vidato vingine.

Dkt. Mahenge alitumia hadhara ya kikao hiko kumshukuru Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa namna ambavyo serikali yake ya awamu ya tano ilivyowekeza fedha nyingi katika elimu kwa kutoa elimu bila malipo kwa ngazi ya shule za msingi na sekondari hadi kidato cha Nne ambapo amesema kwa Mkoa wa Dodoma kwa mwaka wanapokea fedha kwa ajili ya elimu bila malipo zaidi ya shilingi bilioni 3.

“Uwekezaji huu unalenga kumfanya mtoto wa kitanzania asome hadi kidato cha Nne na kuendelea pasipo vikwazo wala bughudha za kiuchumi na mavuno yake uwekezaji huu ni kuona wanafunzi wote wanafikia lengo hilo” alisisitiza Dkt. Mahenge huku akiwataka watendaji wa elimu kusimama imara na kuhakikisha kunakuwa na ongezeko la ufaulu linalouinua Mkoa wa Dodoma na kuuweka katika nafasi ya juu unayostahili kutokana na hadhi yake ya kuwa Makao Makuu ya nchi.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.