• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KONDOA YAJIPAMBANUA KATIKA SEKTA YA AFYA NA KILIMO

Imetumwa : May 4th, 2023

Ziara ya Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo leo tarehe 4 Mei 2023 imeingia siku ya pili ambapo ametembelea Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na kuangazia miradi katika Sekta ya Afya, Elimu na Utawala.

Akiwa Kondoa Bw. Gugu ametembelea miradi saba ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Jengo la Halmashauri hiyo, nyumba ya Mkurugenzi na ujenzi wa nyumba tatu za watumishi. Miradi mingine aliyotembelea ni miradi katika sekta ya Afya  na Elimu.

Katika ziara yake Bw. Gugu ametoa rai kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Bw. Mustapha Semwaiko Yussuf kuhakikisha miradi yote inayoendelea kutekelezwa katika hatua mbalimbali iweze kukamilika ifikapo tarehe 31 Mei 2023.

Serikali imetoa shilingi Bilioni 1.2 kuwezesha ujenzi wa Ofisi na Makao Makuu ya Halmashauri Bukulu na Ujenzi wa Nyumba 3 za Wakuu wa Idara.  Aidha katika sekta ya Afya Bw. Gugu amepongeza hatua nzuri ya maendeleo ya ujenzi wa majengo manne katika Hospitali ya Wilaya ya Kondoa ambayo ni Wodi ya wanawake, wodi ya wanaume, wodi ya Watoto na jengo la kuhifadhi maiti, ambavyo gharama yake ni milioni 750 kutoka Serikali kuu.

Aidha, Bw. Gugu pia amepata fursa ya kutembelea mradi wa ujenzi wa Computer Cluster na ujenzi wa madarasa matatu katika Shule ya Msingi Isabe ambavyo gharama yake ni milioni 80.

Kufuatia ukaguzi huo wa miradi ya sekta ya elimu na afya, Bw. Gugu ametoa maelekezo ya kuhakikisha kuwa miradi yote inakamilika kwa muda uliopangwa na kwa ubora wa hali ya juu.

“Niwahikikishie kuwa tutarudi tena, haya maelekezo tuliyowapa yazingatieni na tutakaporejea tupate taarifa ya utekelezaji wake kwa vitendo” Gugu amesisitiza

Pia, Bw. Gugu amepata fursa ya kuzungumza na watumishi wa Halmashauri hiyo na kuwaasa kufuata misingi na taratibu za utumishi wa umma na kusisitiza kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Awali, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Bw. Mustapha Semwaiko Yussuf amemuhakikishia Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw. Ally Gugu kuwa maelekezo yake yanatekekelezwa kwa vitendo.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.