• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KONGAMANO LA MAOMBI, JAMII YAASWA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

Imetumwa : November 8th, 2022

Wanawake kutoka umoja wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania CCT, wamefanya Kongamano la maombi na uzinduzi wa kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia kongamano linalofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheti Tanzania (KKKT) jimbo kuu Dodoma ambapo Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amealikwa kuwa mgeni rasmi.

Kongamano hilo la siku tatu limeanza Novemba 8 na litaendelea hadi Novemba 10, likiwa na lengo la kupinga ukatili wa kijinsia. Aidha kongamano hilo  linakwenda sambamba na kukabidhi miongozo ya malezi ya Watoto,miongozo iliyozinduliwa hivi karibuni na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, Watoto na watu wenye ulemavu. Mkuu wa mkoa amegawa baadhi ya miomgozo hiyo kwa viongozi na washiriki wa kongamano hilo.

Mhe. Senyamule amesema suala la ukatili wa kijinsia ni mtambuka kwani hata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amelipa kipambele katika kulisimamia kwa kutaka mamlaka husika kuunda sheria kali dhidi ya wanaobainika kufanya ukatili katika jamii.

Aidha, Mkuu wa Mkoa ameainisha matukio ya ukatili wa kijinsia yaliyobainika katika mkoa wa Dodoma kwa kipindi cha mwaka 2021 na robo ya mwaka 2022.

“Kwa mkoa wa Dodoma, mwaka 2021 watu 3,696 walifanyiwa matukio ya kikatili. Mwaka 2022 katika kipindi cha Julai hadi Septemba, Watoto 274 wameripotiwa kufanyiwa matukio ya ukatili na watu wazima 448 ambapo wanaume ni 80 na wanawake ni 368 ikiwa ni jumla ya watu 722” RC ameainisha

Kadhalika, amesema kuwa mkoa wa Dodoma unakabiliwa na changamoto kadha wa kadha zinazopelekea kuwa na idadi kubwa ya watu wanaofanyiwa ukatili ikiwa ni pamoja na mmomonyoko wa maadili, utoro shuleni, ndoa za utotoni, mimba kwa wanafunzi, n.k

“Changamoto ni nyingi ila tushirikiane kuzitatua. Watoto wasipopata elimu kizazi kinaharibika. Mtu anayefanyiwa ukatili hawezi kuwa na amani wala furaha. Sote tuchukue hatua, Serikali ichukue hatua, taasisi za dini zichukue hatua na kila kundi katika jamii lichukue hatua kutokomeza ukatili wa kijinsia katika jamii” Ameongeza

Naye Bi Josephine Mwaipopo, Afisa ustawi wa jamii Mkoa, ameongelea zaidi ukatili kwa upande wa Watoto kwa kufafanua vifungu vya sheria vinavyolinda haki za Watoto.

“Mtoto ana haki ya kuhudumiwa kwa mujibu wa sheria ambapo kifungu namba 8 cha Sheria kinazungumzia haki za mtoto anazopaswa kuzipata kutoka kwa mzazi au mlezi wake. Mtu yeyote anayebainika kufanya ukatili kwa mtoto, kwa mujibu wa sheria anakabiliwa na adhabu ya kifungo cha miaka 6 jela na faini” Amesema Bi Mwaipopo

Kongamano hilo lilitanguliwa na mjadala kutoka kwa wataalamu wa sheria ambao walijadili namna matukio mbalimbali ya kikatili yanavyotokea kwenye jamii zetu na kuona kuwa wazazi wakisimama imara kwenye familia zao, suala la ukatili litakwisha. Wataalam hao wameongeza kuwa wote wanaume na wanamke wakisimama, tunaweza kupinga ukatili wa kijinsia.

Jumuiya ya CCT imeundwa na makanisa 12 ambayo yameunganisha nguvu ili kuwa na sauti ya pamoja na imekua ikishirikiana na Serikali kwenye mambo mengi ya kutoa huduma kwa jamii ikiwemo huduma za kiroho kupitia mafundisho ya Neno la Mungu inayotolewa kwenye makanisa yake, shule, hospitali na kuandaa makongamano kama haya yenye dhumuni la kuisaidia Serikali kupambana na matukio mbalimbali yanayojitokeza katika jamii zetu.

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA MAKUNDI MBALIMBALI MKOANI KWAKE

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.